Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Watu wengi
duniani wametajirika kutokana na vipaji walivyonavyo wakiwemo Wanamuziki,Waigizaji,Wachoraji
,Wabunifu ,Wagunduzi na Wavumbuzi wa mambo mbalimbali.
Watu
waliogundua uwezo walionao ,upekee na umaalumu na kuutumia kwa manufaa yao nay
a jamii yao ndo waliofanikiwa zaidi kwenye ulimwengu wa leo.
Vipaji
walivyonavyo vimegeuka kuwa mashine ya kuzalishia fedha na kuwapa kuishi maisha
wanayoyataka.
Ukifanya
uchaguzi utagundua kuwa watu wenye
vipaji wanalipwa vizuri kuliko watu walioajiriwa .
Kipaji
hakizeeki wala kustaafu ,Leo hii Wanamuziki kama King Kiki,Msondo ngoma bado
wanafanya muziki na kujiingizia kipato wangekua wameajiriwa serikalini tayari
wameshavuka muda wa kustaafu wangekua wako nmajumbani wanakula pensheni na wengine kuugulia ugumu wa maisha.
Kipaji
kinaweza kukupa maisha unayoyataka tofauti na kazi ya kuajiriwa inakulazimu
kuishi maisha kulingana na mshahara unaoupata.
Ndugu yangu
usidharau kipaji ulichonacho kwani ni kitu cha thamani sana na cha pekee na cha
tofauti ambacho si kila mtu anacho isipokua wewe.
Kila mtu
duniani ana kipaji ama uwezo Fulani wa
kipekee na maalumu .Hakuna mtu
aliyeumbwa kama kasha tupu lisilo na kitu .
Una kitu cha thamani ndani yako
jiamini,jikubali,jiongeze kwa kuchukua hatua kutumia kipaji ulichonacho
kubadilisha maisha yako.
Kipaji
kinapaswa kukuzwa kama mche wa mti kwa kumwagiwa maji,mbolea na kupata mwanga
ili kiweze kukua ,kustawi na kuzaa matunda ,matunda ambayo ni mafanikio,fedha,umaarufu, utajiri
na vingine vingi.
Lazima kuwe
na mazingira bora ya kuvumbua na kukuza vipaji kuanzia kwa watoto wadogo,vijana
na hata wazee vipaji vyao vinaweza kuwa rasiliamali muhimu na tunu kwa taifa.
Kutengeneza
mazingira rafiki yanayoruhusu vipaji vya watu kujitokeza na kuonekana nje mithili ya kuku anayetaka kutaga lakini ni
juu yam awe anaweza kutaga yai likapasuka.
Tengeneza
Mazingira bora ya kugundua ,kukuza na kuendeleza vipaji kwa faida ya
jamii,taifa na dunia kwa ujumla.
0765938008
Post a Comment