Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasili
kwenye hoteli ya Ramada Resort akiambatana na Mkurugenzi wa Lino
International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania,
Hashim Lundenga (kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amezindua
rasmi msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka
2016 katika hafla ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Hotel ya Ramada
Resort iliyopo eneo la Kunduchi, Dar es Salaam.
Uzinduzi
huo umewakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo wakiwemo
wabunifu wa mavazi, warembo waliowahi kushika taji la Miss Tanzania
miaka iliyopita na mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania
katika ngazi mbalimbali hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss
Tanzania, Hashim Lundenga akitoa mukhtasari wa mashindano hayo kwa mwaka
huu 2016 kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye (wa pili kushoto). Kushoto ni Mlezi wa kamati ya Miss
Tanzania ambaye pia ni Balozi wa Tanzania nchini Botswana, Mh. Emmanuel
Ole Naiko na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto)
akifurahi jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania.
Kutoka
kushoto ni Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima, Miss Tanzania
1999, Hoyce Temu pamoja na Miss Tanzania 2008, Nasreen Kareem
wakimsikiliza Waziri Nape Nnauye (hayupo pichani).
Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu katika ubora wao.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akiendelea na mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania na
Wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi rasmi.
Kikundi
cha sanaa cha Wanne Star kikitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi
wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 iliyofanyika
mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Ramada Resort ya jijini Dar es
Salaam.
Miss
Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima na wadau wa tasnia ya urembo
wakitazama burudani mbalimbali zilizokuwa zikijiri katika hoteli ya
Ramada Resort ulipofanyika uzinduzi huo mwishoni mwa wiki.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili
kushoto), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa
shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) pamoja
na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey
Mngereza wakishuhudia burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea
ukumbini hapo.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss
Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Waziri
Nape (hayupo pichani) kuzindua msimu mpya wa mashindano hayo.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa
baraka kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss
Tanzania 2016 uliofanyika katika hoteli ya Ramada Resort jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza
wakishuhudia uzinduzi wa nembo mpya ya mashindano ya Miss Tanzania 2016
yaliyobeba kauli mbiu ya "Mrembo na Mazingira Safi"
Pichani
juu na chini ni wadau wa tasnia ya urembo na wageni waalikwa
waliohudhuria uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss
Tanzania 2016.
Msanii
wa Bongo flava, Linah Sanga na ma-dancers wake wakitoa burudani kwenye
uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
Msanii wa Bongo Flava, Linah Sanga katika ubora wake.
Wajumbe wa kamati ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi Waziri Nape Nnauye (hayupo pichani).
Post a Comment