Home
»
KIMATAIFA
» UJUMBE KUTOKA KWA BI. IRINA BOKOVA, MKURUGENZI MKUU WA UNESCO, KATIKA SIKU YA USHAIRI DUNIANI, 21 MACHI 2016
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova.
Shakespeare,
mwandishi maarufu kutoka Uingereza aliyefariki yapata miaka 400
iliyopita, aliandika katika tamthilia yake inayojulikana kama “A
Midsummer Night's Dream” kuwa, “Jicho la mshairi, hutazama kwa umakini
na undani, kutoka mbinguni hadi duniani, na duniani hadi mbinguni. Na
kama vitu vya kufikirika vusivyofahika vinavyoumbika katika mawazo,
ndivyo kalamu ya mshairi inavyogeuza mawazo hayo kuwa katika maumbo
yasiyoweza kudhaniwa”
Kwa
kuwatambua na kuwaheshimu wanaume na wanawake, ambao chombo chao pekee
ni uhuru wa kujieleza, watu wanaofikiria na kuchukua hatua, UNESCO
inatambua thamani ya ushairi kama ishara ya ubunifu wa mwanadamu. Kwa
kutoa umbo na maneno kwa mambo ambayo katika hali ya kawaida hayakuwa
nayo, kama vile uzuri usiopimika unaotuzunguka na mateso na taabu kubwa
za dunia, mashairi yanachangia upanuzi wa ubinadamu wetu, kwa kusaidia
kuongeza nguvu za ubinadamu wetu, mshikamano na kujitambua.
Sauti
zinazobeba ushairi husaidia kukuza upana na utofauti wa lugha na uhuru
wa kujieleza. Sauti hizi hushiriki katika jitihada za kimataifa kuelekea
elimu ya kisanii na usambazaji wa utamaduni. Wakati mwingine, neno la
kwanza la shairi latosha kabisa kurejesha kujiamini pale mtu anapokuwa
anakabiliwa na upinzani na kupelekea kuiona tena njia ya matumaini pale
unapopambana na unyama. Katika zama hizi za teknolojia na uharaka wa
maisha ya kisasa, ushairi hufunya nafasi kwa ajili ya uhuru na
kuvinjari, hali iliyo ndani ya utu wa mwanadamu. Kutoka Arirang za huko
Korea hadi Pirekua za Mexico, nyimbo za Hudhud za jamii ya watu wa
Ifugao, Alardah za Saudi Arabia, Koroghlu za jamii ya watu wa
Turkmenistan na maeneo ya Iran na Afghanistan, na Aitysh za watu wa
Kyrgyz, kila utamaduni una aina ya sanaa yake ya ushairi inaoutumia
kupeleka na kusambaza maarifa, maadili ya kijamii na kiutamaduni na
kumbukumbu za pamoja, ambayo huimarisha kuheshimiana, mshikamano wa
kijamii na kutafuta amani.
Leo
hii, nawapongeza washairi, wasanii, waghani, na wale wote ambao sauti
zao, bila ya wao wenyewe kujulikana, wamejitoa, kwa na kupitia ushairi,
kutoa masomo katika hali ya taswira au ya uwazi, katika bustani au
katika mitaa. Ninatoa wito kwa nchi wanachama wote wa UNESCO kuunga
mkono juhudi hizi za ushairi, ambao una uwezo wa kutukusanya pamoja,
bila kujali asili au imani, kwa lile lililo hasa katika kiini cha
ubinadamu
About Author

Advertisement

Related Posts
- RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE ASHINDA TUZO YA KIONGOZI WA AMANI NA USALAMA WA MWAKA 2023 YA JARIDA LA UONGOZI WA AFRIKA16 Mar 20240
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akikabidhiwa tuzo yake na Waziri wa Mapato wa Jamhuri ...Read more »
- FRIEDKIN CONSERVATION FUND WATOA MILLIONI 84 KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO KWA JAMII YA MOYOWOSI, UVINZA NA UGALA02 Oct 20180
Baadhi ya wakurugenzi na viongozi wa Friedkin Conservation Fund wakiwa katika maonesho ya na...Read more »
- Kijana Aliyemuokoa Mtoto Toka Ghorofani Aanza Kazi Katika Jeshi la Zimamoto31 May 20180
Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita maisha ya Mamoudou Gassama, k...Read more »
- Ndege ya Malaysia iliyopotea na watu 298 mwaka 2014 ilipigwa na Kombora25 May 20180
Taarifa mpya ya kuifahamu leo May 25, 2018 ni kuhusu Wapelelezi wa Uholan...Read more »
- Papa Francis Ataka Kanisa Lifunge Kuombea DRC, Sudan Kusini23 Feb 20180
Papa Francis ametangaza Ijumaa ya Februari 23 kuwa siku ya kufunga na sala kwa ajili ya kuziombea...Read more »
- Arsene Wenger Afungiwa na Chama cha Soka cha England06 Jan 20180
Chama Cha soka cha England FA kimetangaza kumfungia kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene We...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.