Mkurugenzi
wa Masoko, Utafitti na
Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.
Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20
ya benki ya utendaji wa benki hiyo uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
**************
BENKI ya CRDB imelipa kodi ya sh. bilioni 107 kwa
serikali hadi Desemba 31,2015.
Akizungumza na baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa benki
hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya miaka 20 ya utendaji wa benki hiyo,
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Charles Kimei alisema wamefanikiwa kuifanya taasisi
hiyo kuwa kinara wa kutoa huduma bora.
Alisema amana za wateja wa benki hiyo zimeongezeka zaidi
ya mara 100 kutoka sh. bilioni 40 walizoanza nazo mwaka 1996 hadi sh. trilioni
4.2 iliyokuwepo Desemba 31 mwaka jana.
“Safari ya miaka 20 ilikuwa na misukosuko ikiwemo kupata
hasara y ash. bilioni 1.8 mwaka 1997 lakini tunajivunia kusema tumepita salama
na sasa tumekuwa taasisi bora ya fedha hapa Tanzania.
“Idadi ya bidhaa zetu, wateja na hata thamani ya benki
pia imeongezeka… tunao waajiriwa 2,682 wenye nidhamu,” alisema Dk. Kimei huku
akibainisha kwamba katika kampeni hizo watawekeza zaidi kwenye elimu.
Alisema maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka 20 ya
CRDB yatakayohitimishwa Juni mwaka huu yamepewa kauli mbiu ya ‘Benki inayokua
na kuboresha maisha ya watu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki hiyo uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Dk. Charles Kimei (kushoto).
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakishuhudia uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 ya benki ya CRDB katika hoteli ya Ramada leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charls Kimei (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja,
Saugata Bandyopadhyay (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Esther
Kitoka.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya Pamoja.
Wakurugenzi wakiwa wamepozi kwa picha.
Wakurugenzi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Post a Comment