picha kwa hisani ya maktaba
Na Woinde Shizza,Arusha
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za uchimbaji
katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha kwa
kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo hayo
ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa inaweza
kuhatarisha uhai wa maisha yao.
Katika
kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali ambayo
ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka
yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa
inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani
waliendelea na shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha
Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na
yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa
kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba
kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.
Alisema
kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa la vifo
linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na kanuni .
Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias
Kadabila alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya
mkuu wa wilaya ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala ambapo alisema
kuwa pia iatawasaidia kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na
uchimbaji holela.
Aidha
pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa ushirikiano
ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo kwa muda wa
mwezi mmoja .
Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao ambapo walisema kuwa hawakubaliani
na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji huo ndiyo ambao unawafanya
kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto na kwamba serikali
iangalie namna nyingine.
"kwakweli
tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi wananachi
ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia tunaweza kula
,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha maisha
yetu"Alisema Lowayani Metili
Ipo
haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na
serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati
wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga
wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.
Post a Comment