NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Chama cha
soka wilaya ya Mondoli (MODFA),kinatarajia kufanya uchaguzi Mkuu Mwezi wa pili mwaka huu (2016), ili kupata uongozi kwa nafasi nane zinazowaniwa ili kupata
uongozi utakao kiendesha chama hicho kwa miaka mitatu.
Katibu Mkuu wa Chama cha soka wilayani
humo Twaha Kibayasi, alisema kuwa taratibu kamilihazija kamilika japo mambo yanaenda
vizuri na nafasi nane ndizo zinazowaniwa katika uchaguzi huo.
Nafasi zitakazo waniwa ni Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti, Katibu, Muweka Hazina, Mjumbe wa mkutano Mkuu, Mwakilishi wa
Vilabu na Wajumbe watatu wa kamati tendaji.
“Zoezi la uchukuajiwa wa fomu bado halijaanza
na pindi taratibu zitakapo kamilika tutawatangazia lasmi ikiwa pamoja na ada ya
kila nafasi itakayo tangazwa, cha msingi ni kuwaomba wajitokeze na wawe tayari kugombea
nafasi hizo” alisema Kibayasi
Kwa mujibu wa katiba ya MODFA mtanzania
yeyote mwenye Sifa zitakazo ainishwa ikiwa pamoja na elimu ya sekondari na
kuendelea anafaa kugombea nafasi yoyote.
“Sio sifa hizo pekee Pia asiyewahi kushitakiwa
kwa kosa lolote na kufungwa na awe mpenda michezo ndio sifa mojawapo itakayoangaliwa
maana watu wanapenda kuleta siasa kwenye michezo na mwisho kuhalibu soka”
aliongeza kusema Kibayasi.
Kibayasi alisema kuwa mara baada ya
mwaka mpya Kamati tendaji ya MODFA inatarajia kukaa pamoja na kujadili mambo
mbalimbali ikiwepo juu ya kuandaa ligi ya Wilaya hiyo inayo suasua ili kupata bingwa
atakaye iwakilisha Monduri katika Ligi ya Mkoa wa Arusha inayotarajia kuanza
mapema mwezi januari.
Uchaguzi huo umehairishwa zaidi ya mara
mbili kutokana na sababu mabali mbali ikiwemo watu kutojitokeza kugombea nafasi
zilizotangazwa, uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika mwezi wa tano mwaka uliopita
(2015).
Kibayasi Aliongeza kuwa kwa sasa
wasipojitokeza watafanya uchaguzi kwa nafasi ambazo zitapata wagombea na pia
wataandaa uchaguzi mdogo hadi wajaze nafasi zote kulingana na taratibu na
sheria za MODFA
Post a Comment