NA;
YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Chama cha Mpira
wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA), Kipo katika hatua za mwisho kufanya uchaguzi
Mkuu mapema mwezi huu uongozi utakao kiongoza chama hicho kwa muda wa Miaka
Mitatu.
Mwenyekiti wa
chama cha Mchezo wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA) Barick Kilimba alisema kuwa
nafasi kuu mbili zitagombewa ikiwa pamoja na nafasi ya Mwenyekiti Mkuu, na
Msaidizi wake, Katibu Mkuu na Makamu wake.
“Nilikuwa
naongoza huku nacheza hivyo ilikuwa inaniwia vigumu sana wakati mwingine,
katika kutoa maamuzi nilikuwa naogopa kuonekana napendelea Timu yangu, hivyo
nimeamua niweke uongozi pembeni nibaki kuwa mchezaji pekee”
“Shida ilikuwa
hakuna watu wa kuongoza nafasi hizi lakini tumewashawishi wale wachezaji
wakongwe waje washike madaraka ili watuongoze na kutuonesha wao walikuwa
Wanafanyaje kipindi wao wanacheza” Alisema Kilimba.
Aliongeza kuwa
wanatarajia kufanya kikao cha viongozi wote Waliokuwa madarakani kwa sasa ili
kupanga tarehe maalumu ya kufanya uchaguzi huo, ikiwa pamoja na kutangaza sifa
za wagombea.
Pia ARBA
Wanatarajia kuendesha Bonanza la mchezo huo kwa kushirikisha timu zote
zinazopatikana Mkoani hapa pamoja na mikoa ya Jirani ikiwa na Lengo kupanua na
kutangaza Mchezo huo katika ukanda wa Kusini.
Kilimba alisema
kutoshirikiana baina ya viongozi ndio sababu kubwa ya Mchezo huo kufifia Mkoani
hapa, kwa iongozi wengi kukwepa majukumu yao na kuwa Bize na mambo yao Binafsi.
Hata hivyo
alikiri ARBA kukabiliwa na ukata kitu ambacho kilisababisha kushindwa kushiriki
mashindano ya Kitaifa yaliyokuwa yanafanyika Mkoani Dodoma mwezi Disemba mwaka
uliopita, licha ya kukiandaa kikosi.
Post a Comment