NA; YOHANA CHANCE.
ARUSHA.
Timu ya Rhino Rangers kutoka Mkoani Tabora
imefanikiwa kuvunja rekodi ya JKT Oljoro
waliyoiweka katika ligi daraja la kwanza (FDL),katika mchezo uliopigwa mwishoni
mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Oljoro haijafungwa wala kutoka Sare mchezo
hata mmoja tangu kuanza kwa ligi daraja la Kwanza, kabla ya Rhino kuivuruga
Rekodi hiyo mwishoni mwa wiki, Oljoro walifungwa Mchezo wa ufunguzi wa ligi
hiyo dhidi ya Panone Fc katika uwanja wa Ushirika Moshi na kisha kutoka sare ya
bao 1-1 na JKT Kanebwa Mkoani Dodoma.
Katika mchezo huo Wenyeji Oljoro
walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 16 kupitia kwa Shaibu Nayopa kwa njia
ya Mkwaju wa Penati baada ya Paulo Malipesa kuangushwa eneo la hatari na Ismail
Msikilwa.
Rhino waliongeza juhudi zaidi kipindi
cha Pili na kufanikiwa kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mchezo
kumalizika kupitia kwa Ramadhani Mwinyimbegu, mchezaji ambaye alishawahi
kukitumikia kikosi cha Oljoro kabla ya kutimukia Rhino.
Mara baada ya Mchezo wa huo JKT
Oljoro watakuwa Wanaanza kutoka Nje tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi
hiyo,kucheza na Mbao mkoani Mara, na Kwa
matoko hayo JKT Oljro wanakuwa wamefikisha Pointi 18
Post a Comment