Mrembo maarufu aliyependezesha video ya 'Furaha' ya Young D, Tunda 76
amedai kutajwa kwake kwenye orodha ya wanaohusika na dawa za kulevya
kumempa changamoto ya kuaminika nyumbani kwa wazazi wake.
Tunda amezungumza hayo kwenye eNewz ya EATV na kusema kuwa tangu
kutajwa kwenye wahusika wa matumizi ya madawa imemfanya kubadilisha
mpaka mfumo wa maisha kwa kuwa nyumbani kwa wazazi wake wamekuwa wagumu
kumuelewa.
"Nimebadilisha mfumo wa maisha, naishi maisha ya low profile kwa sasa
ili mambo kwanza yatulie lakini nipo. maisha ya mitandaoni nimeacha.
Suala la kutajwa linaniumiza kwa sababu nyumbani haikuwa rahisi
kueleweka na wazazi.
Viongozi wanadai natumia mimi ndo niseme najitetea ukweli ni vigumu mno
lakini naamini kwenye ukweli uongo hujitenga pembeni ipo siku ukweli
utajulikana na maisha yataendelea kama kawaida. Niweke wazi situmii
madawa ya kulevya". Alisema Tunda
Tunda na baadhi ya mastaa wengine wapo nje kwa dhamana baada ya kutuhumiwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya.
Post a Comment