PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU LETICIA NYERERE
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Balti...


Misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutok kila kona ya Marekani. Mwili wa marehemu Leticia Nyerere unatarajia kufika Tanzania leo  Jumanne January 19, 2016 na utaagwa Dar es Salaam na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Butiana. Picha na Iska Jojo.
Wana familia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Bi. Kijogoo kutoka Arizona,,Margareth Mageni na ,Flora Mageni
Wanafamilia wakiwemo watoto wa marehemu kutoka kushoto ni Julius Nyerere, Helena Nyerere na Julia Nyerere kulia ni Edlaila  Nyerere ambaye ni wifi wa marehemu kutoka Atlanta jimbo la Georgia nchini Marekani  wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa mama yao Leticia Nyerere aliyeaga Dunia siku ya Jumapili January 10, 2016 katika hospitali ya Jumuiya ya Madaktari iliyopo Lanham, maryland nchini Marekani.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akitoa mkono wa pole kwa mume wa marehemu Madaraka Nyerere kwenye misa ya kumbukumbu  ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki

Balozi Wilson Masilingi akiongea machache na kutoa pole kwa wafiwa.

Bi Resty Budodi Semali rafiki wa marehemu kutoka Atlanta akiongea jambo ya jinsi alivyomfahamu marehemu.

Bhoke Nyerere kutoka Canada akisoma neno.
 daktari wa familia Dr. Ndubisi akiongea jinsi alivyomfahamu marehemu.
Katibu mwenezi wa CCM DMV akielezea jinsi gani alivyomfahamu marehemu
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na kuelezea jinsi gani alivyomfahamu marehemu.
Pius Mtalemwa mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Wakatoliki DMV akisema machache ya jinsi alivyomfahamu marehemu.
Watoto wa marehemu kutoka kushoto ni Julia, Julius na Helena.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top