Mkubwa wa kazi ambaye amewahi kushika nafasi kubwa za
uongozi katika taifa hili na mwenye kasi ya ajabu katika medani za
siasa, uchumi katika chama chake, amekuwa akiwaonya wapinzani wake
kutotumia kete ya mali zake kama njia ya kumchafua ki siasa.
Amesema hapendezwi na hilo, na jambo hilo halina tija kwa
siasa zetu za Tanzania, kuna mijadala mingi ya ki taifa ya kujadili kwa
maendeleo yetu na siyo mali zake kwani anazo mali za kawaida kuliko
inavyozushwa.
Kakazia kwamba wapinzani wake wasijikite katika mali zake kwani "ALIYEPATA AMEPATA".
Haya wadau hizi ndiyo siasa za bongo watu wamewekeza kwenye kuchafuana tu.
Post a Comment