KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameelezwa kufurahishwa
na jitihada za kumaliza mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar,huku akitaja
baadhi ya mbinu ambazo chama chake waliishauri Serikali ambazo zimeanza
kuchukuliwa hatua.
Hii hapa chini ni post yake katika mtandao wa facebook juu ya suala hilo
Zanzibar taratiibu….
Disemba 20 mwaka huu 2015 Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo ilitoa tamko lake baada ya kufuatilia hali ya Zanzibar.
Moja ya mambo yaliyoelezwa katika tamko hilo ni uwepo wa askari wengi
katika kisiwa hicho hali iliyokuwa inatishia amani kwa wananchi
Taarifa hiyo ya ACT mbali na masuala mengine, ikaeleza kuwa ni wakati
muafaka kwa serikali kuhakikisha inawarudisha askari hao wa vikosi mbali
mbali kuanzia jeshi la Polisi,JKU,KMKM JWTZ na Mafunzo katika makambi
yao.
Lengo likiwa ni kuwaacha wananchi wakiwa katika uhuru wa kufanya
shughuli zao wakati suala la mtanziko wa kisiasa kisiwani humo ukiwa
unafanyiwa kazi
Kuanzia jana Disemba 22 na leo Disemba 23 majeshi hayo yameshaanza
kuondoka katika maeneo mbali mbali ya mji wa Znz hali inayoashiria
mwanzo wa mwisho mwema katika kadhia ya uchaguzi wa Zanzibar.
Ninaomba mamlaka husika ziendelee kufanyia kazi mapendekezo yetu mengine ili kulimaliza kabisa suala hili.
Post a Comment