Rapa huyo mkongwe aliyekuwa kimya kutokana na shughuli za kampeni, ameiambia Bongo5 kuwa anaamini wasanii wanaosafiri kwaajili ya kushoot video nje, wana bishara zao za siri.
“ Kwenye kushoot video nje ni ulimbukeni,” amesema.
“ Tanzania tuna kila kitu kuliko hata huko wanakoenda. Mimi hii naitafsiri ni usaliti wa nchi, sisi tunakosa nini hapa nyumbani? Tuna milima, mbuga, maporomoko mazuri, yaani tuna kila kitu. Unajua wasanii wengi walikuwa wanatumia mwanya wa kwenda kushoot video nje ili kufanya biashara zao za siri. Wengi wameutumia sana huu mwanya, sasa Magufuli alivyoingia atawanyoosha tu,” amesisitiza Afande.
Katika hatua nyingine Afande Sele amesema anajipanga kuachia nyimbo mpya mbili ili kufidia ukimya mkubwa aliouacha kwa mashabiki wake.
Post a Comment