PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JKT OLJORO YATOLEWA MICHUANO YA FA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Na; Yohana Challe ARUSHA. Timu ya JKT Oljoro imetolewa katika michuano ya FA inayoendelea hapa nchini, baada ya kukubali kufun...
 
Na; Yohana Challe
ARUSHA.

Timu ya JKT Oljoro imetolewa katika michuano ya FA inayoendelea hapa nchini, baada ya kukubali kufungwa na timu ya Mdini FC inayoshiriki ligi daraja la Pili kwa mikwaju ya penati 7-6, mchezo uliochezwa ktika uwanja wa Sheikh Amri Abeid juzi jumatano.

Hatua ya Mikwaju ya Penati ilikuja baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 bila kufungana ndipo mikwaju ya penati ikamuliwa kupigwa.

Waliopiga penati kwa upande wa Oljoro ni Paulo Malipesa, Lawrence Milton, Shaibu Nayopa, Swalehe Hussein, Abdul Ibadi, Said Mashaka wote wakiwa wamefunga penati zao wakati Lucas Charles Mkwaju wake uliota mbawa baada ya kudakwa na Golikipa wa Madini Sebashar Stanley.

Kwa upande wa timu ya Madini walioipa ushindi timu hiyo baada ya kupiga mkwaju yao na kupata zote ni pamoja na Wilson Mollel, Edward Kang’ori. Ramadhan Ntobi, Lesika Lekindoki, Fred Paulo, Juma Juma na Priscus Julius.

Mara baadaya ya mchezo huo Kocha wa JKT Oljoro Joery Mwambegele alisema kuwa bahati haikua yao, hivyo kwa sasa wanaelekeza nguvu kwenye ligi daraja la kwanza hasa mzunguko wa pili utakaonza Mwishoni mwa mwezi huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top