Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Wiliam Ole Nasha akishukuru kwa
uteuzi wa Rais John Pombe Magufuli katika baraza la Madiwani wa
halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ,Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Arusha Daudi Felix Ntibenda,Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Hashim na
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mathew Siloma.Picha na Ferdinand Shayo
Naibu Waziri
Mteule wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi William
Ole Nasha amesema kuwa hatamwangusha Raisi John Pombe Magufuli na Watanzania
kwa kuhakikisha kuwa anawajibika na kufanya kazi kwa bidii na kuleta mabadiliko
katika sekta hizo .
Nasha ambaye
uteuzi huo ulivyotangazwa rasmi kwenye
vyombo vya habari ulimkuta katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya
ya Ngorongoro hali iliyowashangaza wengi kwani hawakuwa wametarajia kuwa uteuzi
huo ungetokea.
Akizungumza
katika baraza la Madiwani Nasha alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kuwa hatawaangusha
Watanzania kuwa hana rekodi ya kukosa
maadili.
“Umakini mkubwa
umetumika kuteua baraza la Mawaziri mpaka leo hii Mheshimiwa Raisi hajamaliza
kuteua baraza , ni heshima kubwa sana kwangu namshukuru Magufuli kwa dhamana
hii kubwa “ Alisema Nasha
Nasha
amesema kuwa atashirikiana na wataalamu kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo
katika taifa la Tanzania.
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Daudi Felix Ntibenda ambaye alikuwepo wilayani hapo katika ziara yake
ya kikazi ya siku 3 amempongeza Mbunge huyo wa Ngorongoro ambaye kwa sasa ni
Mbunge Mteule wa Ngorongoro.
Ntibenda
amesema kuwa anaamini kupitia uteuzi huo utasaidia kuinua sekta ya ufugaji
kutoka kwenye ufugaji wa kienyeji hadi kwenye ufugaji wa kisasa utakaoleta tija
na kuinua uchumi wa wafugaji na taifa kwa ujumla.
|
Post a Comment