NA;
YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu ya AFC
imeapata kuisambaratisha timu ya JKT Rwankome katika mchezo wa mwendelezo Ligi
Daraja la Pili Ngazi ya Taifa (SDL), Utakaochezwa jumamosi hii hapa
jijini Arusha Katika dimba la Sheikh Amri Abeid.
AFC yenye makazi
yake jijini Arusha haijafanikiwa kupata pointi hata moja tangu kuanza kwa Ligi
hiyo , kwani katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Pamba walichezea kichapo cha
bao 3-0 kisha mwishoni mwa wiki iliyopita wakilala kwa bao 2-0 dhidi ya
Alliance FC ya Jijini Mwanza.
Hata hivyo AFC
imekuwa katika hali isiyolidhisha hasa katika michezo ya awali ikisemekana
kufanyiwa hujuma na baadhi ya vingozi wa chama cha Soka Mkoni hapa (ARFA) wakishirikiana
na wachezaji wachache.
AFC katika mchezo
wa kwanza dhidi ya Pamba wakiwa mkoani Mwanza walijikuta wakiingia uwanjani
huku katika benchi la akiba Akibaki mchezaji mmoja pekee.
Katibu mkuu wa
AFC Salim Kombo alisema kuwa tayari matatizo hayo yameshatatuliwa na kwa sasa
wanaanza kuhesabu pointi katika mchezo wa kesho dhidi ya JKT Rwankome ili
kufanikisha lengo la kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
AFC inajumla ya
kikosi cha wachezaji 22 huku wawili wakiwa masomoni ambao ni Humphrey Willium
akiwa Chuo cha DIT,na Julius Mwajebele akiwa SUA Mkoani Morogoro.
Sambamba na hilo
Katibu Msaidizi wa AFC Charles Mwaimu aliongeza kuwa kuna wachezaji sita wa
kikosi hicho wanarubuniwa ili wasiichezee AFC ili hali walishasajiliwa.
“Wachezaji tunaowengi
ila wanarubuniwa mfano Aldina Hashim, ,Madaga Luke, Gibson Chuma, Steven
Mwakalinga, Samson Mwaluka, na Mohamed Juma” Alisema Mwaimu.
Post a Comment