NA;
YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu
kutoka Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu imefanikiwa kutwaa ubingwa katika
michuano ya SHIMMUTA ilimalizika mwanzoni mwa wiki hii jijini Hapa.
Timu
hiyo imefanikiwa kutangazwa kuwa mabingwa baada ya kunyakua vikombe vingi
katika michuano hiyo iliyokuwa inajumuisha zaidi ya michezo 12 na zaidi ya Timu
20 zilijitokeza katika michuno hiyo iliyofanyika kwa siku tano tangu Setemba 26
hadi septemba 30 mwaka huu.
Michezo
ilikuwa inashindaniwa ni pamoja na riadha, kuvuta kamba, Mpira wa Pete, Mpira
wa Kikapu, Mpira wa Miguu, Drafti, kukimbia na gunia, Bao,na mchezo wa vishale.
Timu
shiriki ni pamoja na vyuo mbali mbali ikiwemo SUA, UDOM, UDSM, MUHASI, ATC,IAA,
MUCCobs, Ardhi, na Mzumbe, pia taasisi na makamuni mbalimbali yalikuwepo
yakishiriki ni pamoja na TANESKO, TANAPA, TBS,NEMC, Mipango, TPDC, AICC, na
AUWASA.
Mgeni
rasmi katika ufungaji wa michuano hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili
Nkuru ambapo alisisitiza na kuwasihi wanamichezo kudumisha fani zao hata
wanapokuwa sehemu zao za kazi.
“Michezo
huleta watu pamoja kwa umoja, ushirikiano, na umoja mfano mzuri mnaona hapa
watu wametoka Mbeya, Mwanza na wengine Dar es Salaam, lakini wote tumekuwa kitu
kimoja”Alisema Nkuru
Aidha
Katibu mkuu wa SHIMMUTA Award Safari alisema kuwa licha ya kupokea malalamiko
kutoka sehemu mbalimbali juu ya mashindano hayo hasa katika timu ya shirika
kuchezesha mamruki watalifanyia kazi katika mashindano yajayo.
“Pia
Uongozi wa SHIMMUTA umesikitishwa na uongozi chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kwa
kuitoa timu isiendelee kushiriki katika ya michuano hii kwani imeleta usumbufu
kutokana na kuwa ilikuwa tayari imeanza mashindano “aliongeza safari.
Post a Comment