PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MOUNT MERU MARATHONI KUFANYIKA OKTOBA JIJINI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIA TZ Mashindano ya riadha yajulikanayo kama Mount Meru Marathon yanatarajia kufanyika oktoba 4 mw...
Image result for mount meru marathon



Mashindano ya riadha yajulikanayo kama Mount Meru Marathon yanatarajia kufanyika oktoba 4 mwaka huu jijini hapa kwa kushirikisha wanariadha kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza na gazeti hili Mratibu wa mashindano hayo Gidamis Shahanga alisema kuwa mashindano hayo yataanzia mnara wa saa na kwenda uwanja wa ndege na kuhitimishwa katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

“mashindano haya chimbuko lake ni mkoani hapa na mara ya mwisho kufanyika ilikuwa mwaka 20000 kipindi hicho yakiwa yanaitwa , Mount Meru International Marathon, hivyo tulisimama kutokana na mambo kuto kuwa mazuri hasa kwa upande wa fedha” alisema Shahanga.

Shahanga ambaye pia ni katibu wa Chama cha Riadha mkoani hapa, aliongeza kuwa mashindano hayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali, kutakuwa na mbio za 21km ambapo mshindi atajinyakulia kiasi cha sh 200,000.

Pia kutakuwa na mbio za 5km ambazo hakuweza kuweka bayana zawadi ya mshindi huku akisisitiza kuwa 5km zitakuwa kwa watu maalumu kama vile wazee.

Mashindano hayo ni ya wazi ambapo mtu yoyote anaruhushiwa kushiriki hata kama sio mtanzania, ilimradi amefuata taratibu na kanuni zote zitakazowekwa ikiwa pamoja na kujiandikisha kwa muda muafaka.

Mashindano hayo yanaandaliwa na kampuni ya Mambo leo Digital Centre kwa kushirikiana na chama cha riadha mkoa wa Arusha, huku wadhamini wakuu wakiwa ni SBL.

Usajili kwa washiriki utaanza septemba 20 na kumalizika Oktoba 3 jioni katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, na Arusha Hoteri ambao pia ni wadhamini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top