PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA YA LEO: USALAMA WA TAIFA UPO MIKONONI MWA WANANCHI.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA; YOHANA CHALLE.PRINCEMEDIATZ.   0762 801099, 0652 362138 Nchi yoyote haiwezi kuendelea pasipokuwepo na usalama madhub...
Image result for ramani ya tanzania

 Image result for princemedia tz logo

Nchi yoyote haiwezi kuendelea pasipokuwepo na usalama madhubuti kwa taifa lake, maana kuwepo kwa usalama kutawafanya wananchi kuishi kwa Amani na kujiamini pasipokuwa na wasiwasi wowote wa vitendo vitakavyo vunja Amani.

Taifa lenye Amani ya usalama mzuri halitegemei Jeshi ili kuleta Amani, wala halitegemei mtu Fulani, au kiongozi Fulani akiwa madarakani au akiingia madarakani basi ataweza kuleta usalama kwa taifa, laah hasha! Bali RAIA wa taifa lenyewe ndilo wenyewajibu wa kulinda nchi yao.

Asilimia kubwa ya usalama wa taifa inabebwa na RAIA kwa sababu wao ndio miongoni mwa jamii na ndio wengi kuliko hata dola, na ndio wenye nguvu kuliko hata jeshi bali jeshi ni sehemu tu ya kusimamia usalama wa Taifa.

RAIA mwema kwa taifa lake hapendi kuona amani ya taifa lake inavulugwa na mtu,watu au kikundi kwa manufaa yao binafsi hasara ikawa kwa taifa zima.

RAIA mwema hapendi kuwa mkimbizi ndani ya taifa lake, kwani ni aibu kubwa kuomba AMANI ukiwa katika taifa lako , ni fedhea kuomba sehemu ya kujihifadhi ukiwa ndani ya nchi yako, ni vibya kuwa mtumwa ukiwa ndani ya nchi yako.

Lakini hayo yote yanawezekana kutokea endapo mimi na wewe tusipo ilinda tunu ya AMANI tuliyopewa na mwenzezi Mungu kwa muda mrefu, japo wahenga walisema kujenga ni vigumu bali kubomoa ni rahisi.

Ndugu zangu watanzania AMANI hii tunayojivunia kumbuka waliyoijenga wengi wamefariki na ni katika harakati za kuijenga AMANI hii wengi walipoteza maisha, hivyo tukumbuke kuwa tukiibomoa basi tuwe tayari kupoteza watu kwa ajili ya kuijenga Upya AMANI hii.

Ukiangalia siasa inavyoendelea katika nchi yetu utakuwa na jibu tosha juu ya AMANI ya taifa hili, kuwa kiongozi ni haki ya kila mtu, kupiga kura ni haki ya kila mtu, kumchagua kiongozi ni haki ya kila mtu. Lakini kumbuka haki haiji bila kuwajibika.

Katika katiba ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 sura kwanza sehemu ya tatu, kifungu cha 17 (1) kinasema “kila raia wa jamuhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamuhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote,kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jmuhuri ya Muungano”

Mtanzania mwenzangu hayo yote yanaweza kuwa ndoto endapo hatutashiriki kikamilifu katika ulinzi wa Taifa hili taijiri kwa AMANI.

Nchi kuwa na AMANI au vita haitaji kuangalia kabira, elimu, wala Dini Fulani, maana hali ikiwa mbaya kila mmoja ataona uchungu wake na kusahau hata kama una nyumba nzuri, gari zuri au una pesa nyingi maana wote tutalala porini.

Ukiangalia katika katiba ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 sura ya sita sehemu ya kwanza, kifungu cha 130 (1) kupitia tume ya haki za Binadamu na utawala bora itekeleze yafuatayo:



Mambo mengi hufanywa na tume hiyo kwa ajili ya usalama na haki kwa wananchi wake, ila wananchi tuna wajibu mkubwa kuliko hata tume katika kulinda usalama wa taifa letu.

Hata hivyo viongozi wetu wanatakiwa kuwa na mtazamo yakinifu katika kulinda AMANI ya nchi yetu kutokana na nchi zote zinazotuzunguka kuwa katika hali isiyolidhisha kiamani na kimbilio lao ni katika nchi nchi yetu.Je taifa letu likikosa amani tutakimbilia wapi ili tuitwe wakimbizi?

Kwa wale wafuatiliaji wa vyombo vya habari wakubali kuwa kuna ukiukwaji mkubwa katika Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuweka na kuendeleza misingi ya utawala bora.

Kunaonekana na kuwepo kwa upindishwaji wa haki za binadamu, demokrasia na utawala bora wa sheria katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda), na misingi hiyo yote imepewa kipaumbele sana katika nchi hizi.

Hata hivyo nchi yetu imeshawahi kuingia katika mgongano mara kadhaa na nchi hizo zote, hata ambazo azipo katika jumuiya ya Afrika Mashariki ila ni majirani zetu, mafano Nchi ya Malawi na Tanzania waliingia katika mgogoro wa juu ya umiliki wa ziwa nyassa na hadi sasa hakujapatiwa ufumuzi juu ya mgogoro huo japo kwa sasa hali ni shwari.

Pia Rais wa nchi ya Tanzania Jkaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa nchini Rwanda, vyombo vyingi vya habari hapa nchini na huko Rwanda viliwahi kuripoti kuwa wakuu hao waliingia katika hali isiyokuwa ya kawaida kila mmoja akimtunishia mwenzake kifua japo nalo lilikwisha.

Deus Kibambaamaye ni mtafiti na mchambuzi wa jamii aliyebobea katika maeneo ya uhusiano wa kimataifa, katika moja ya maandishi yake aliwahi kusema kuwa:

“kutokana na ufinyu wa malengo ya ujenzi wa utamanduni wa kidemokrasia katika Afrika Mashariki, ukanda huu unaongoza kwa migogoro ya kisiasa ndani na baina ya wanachama kiasi kwamba upo wakati inabidi kujaribu kutumia akili ya kuzaliwa katika kutatua tafrani zinazojitokea kwa kukosa mfumo madhubuti ndani ya Mkataba wa ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika mashariki wa mwaka 2000”

“kwa bahati mbaya, pasipo demokrasia na utawala wa sheria katika nchi wanachama na miongoni mwao, ushirikiano katika Nyanja nyinginezo unakuwa si endelevu na unakuwa unapata tafrani kiasi cha kutikiswa na mawimbi ya utawala wa kibabe kama ilivyotokea wakati wa Nduli Iddi Amin Dada mwishoni mwa miaka ya 1970s hadi kugeuza lengo la ushirikiano la jumuiya”

Nyumba yenye AMANI, UTULIVU NA UPENDO ndiyo inayokuwa na wageni kila mara, vivyo hivyo katika nchi wawekezaji hupenda nchi yenye sifa za namna hii.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top