NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ
Timu
ya kikapu ya Mombasa kutoka nchini Kenya inatarajia kushiriki katika
michuano ya wazi katika mchezo huo yanayoyojulikana kama Kilimanjaro
Basketball Cup yatakayofanyika Arusha kuanzia Septemba 13 hadi 19 katika
viwanja vya Soweto.
Akizungumza
na gazeti hili Mwenyekiti wa chama cha Mchezo wa Kikapu Mkoa wa Arusha
(ARBA) Barick Kilimba alisema kuwa tayari zaidi ya timu kumi kutoka
ndani na nje ya nchi zimethibitisha ushiriki wao.
“zaidi
ya wachezaji 100 kutoka timu shiriki ambazo ni Soweto, Hoo,Spider, na
Internatinal stars kutoka Arusha, Bandari Tanga,JKT Dar es salaam,
Baptist na KCMC kutokaka Kilimanjaro, Morogoro, Zanzibar pamoja na
Mombasa kutoka Nchini Kenya” alisema Kilimba
Mashindano
hayo yanaandaliwa na Shirikisho la Mchezo Kikapu Tanzania (TBF) kwa
kushirikiana na Chama cha mchezo wa Kikiapu Arusha (ARBA).
Kilimba
alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha wanakuza mchezo
huo na kuinua vipaji vipya ambavyo bado havijajulikana zaidi katika
ukanda wa Kaskazini pia kutangaza vivutio vya kilatilii vilivyopo ukanda
huu hasa Mlima Kilimanjaro.
“Michuano
hii ilikuwa ifanyanyike Moshi lakini wenzetu wa Moshi wakatuomba
ifanyike Arusha kutokana na wao kuwa na viwanja vyenye hadhi ya chini
pia Mkoa huo hauna mwamko mkubwa ukilinganisha na Arusha” alisema
Kilimba.
Aliongeza
kuwa mashindano hayo yatafunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Felix
Ntibenda ambaye anaonekana kupenda kukuza michezo katika mkoa wake,
licha ya mashindano hayo kukosa udhamini hadi hivi sasa na kuwaomba
wadau kujitokeza kudhamini mchezo huo.
Post a Comment