PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: THERESIA ALIWEKA HISTORIA ALL AFRICAN GAME 1965
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. PMT Tanzania inakwenda katika mashindano ya All African Game ikiwa na kumbukumbu ya Mtanzania Bi Theresia Dism...

NA; YOHANA CHALLE. PMT


Tanzania inakwenda katika mashindano ya All African Game ikiwa na kumbukumbu ya Mtanzania Bi Theresia Dismas ambaye alileta medali ya kwanza katika ufunguzi wa mashindano hayo nchini Congo Brazzaville mwaka 1965, ambayo kwa sasa yanatimiza miaka 50.

Shujaa huyo kwa sasa anaishi nchini Kenya ambapo aliweza kutwaa medali hiyo baada ya kuibuka mshindi katika zoezi la kurusha Mkuki na kuweka historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuleta medali hapa nchini kupitia mashindano hayo.

Hata hivyo mwanariadha Wilhem Gidabuday alisema kuwa mashindano hayo kwa Tanzania yana historia ya kipekee kupitia Bibi huyo na pia ni fulsa kwa wanamichezo chipukizi kujua historia mbali mbali za mashujaa katika michezo.

Watanzania hasa Baraza la Michezo Tanzania (BMT),wangetumia uzalendo na upendo ili kumjumuisha huyo mama katika Safari ya kuelekea huko Congo” alisema Gidabuday

Aliongeza kuwa wanariadha waliokwenda Congo Brazzaville hawajajiandaa vizuri hivyo watanzania wasitegemee chochote kwasababu ni wanamichezo hao hao waliotoka Nchini China katika mashindano ya Dunia na hawajapewa fulsa ya kupumzika, hivyo kitaaluma ya michezo ni kosa.

Alisisiza kuwa Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa katika idara ya michezo hasa uongozi wa idara ya michezo, wengi hawana uzalendo na sio kwa upande wa riadha pekee.

Akina mama wengi ambao nii Viongozi wanahitaji usawa lakini sijaona wakiumkumbuka mwanamke mwezao kwa kutoa mifano juu ya ushujaa wake alioufanya kupitia michezo lazima wampe nafasi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top