NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ
Kila mtu anandoto ya
kuwa tajiri, maana hakuna anayependa umasikini, kwasababu mtu masikini hata
akiwa na mawazo mazuri hawezi kusikilizwa,na wakati mwingine hata heshima yake hushushwa
na yule tajiri huheshimiwa sana hata kama kwao ni mdogo na hata kama hakuenda
shule hilo halijalishi.
Akina mama wengi ndio
wanaonekana kujikusanya pamoja na kuunda vikundi vidogovidogo vya ujasiliamali
kwa ajili ya kujikwamua kimaisha ya hali ya chini na kufikia angalau watu wa
hali ya kati,huku wakina baba wakionekana kwa mbali sana.
Shirika lilsilo la
kiserikali la Usariver Community Organization (URICO), lililopo wilayani
Arumeru Mkoani hapa ambalo linashuhulika na shughuli mbalimabli ikiwemo kulea
watoto yatima, kwa kutambua umuhimu wa vicoba imeamua kuvikuasanya pamoja
vikundi mbalilmbali katika wilaya hiyo.
Katibu mkuu wa URICO
Daud Lezile alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa akinamama katika jamii
walivikusanya vikundi takribani 23 vilivyopo ndani ya wilaya hiyo ili kuwaweka
pamoja na hatimaye kuwa na kundi moja lenye nguvu.
“katika vikundi
tulivyo vikutanisha hapo awali vilikuwa 23 na vyote viliitikia wito, lakini
vikundi 12 tu ndivyo vilivyokubali kuungana na sisi ni kama wasimamizi wao
katika kufanikisha yale waliyolenga kuyafanikisha” alisema Lezile
URICO inawasaidia
wajasiliamali kupata elimu mbalimbali ikiwemo ya biashara ndogondogo (kuuza
mchele na mboga mboga na chakula), kilimo cha mpunga, mahindi na mboga mboga
ufugaji (ng’ombe, mbuzi na kuku na bata)
Shirika hilo limefanya
juhudi za kuwaunganisha wanavikoba na hatimaye kuwa kikundi kimoja
kijulikanacho kama Muungano wa Vicoba Usaiver (MUVIU), ambapo kikundi
kinawasaidia kupata mikopo katika taasisi za kifedha.
Licha ya kupata mikopo
MUVIU inasaidia wajasliamali kubadilishana mawazo na kuelezea uzoefu walionao
baadhi ya watu mbalimbali,kuendesha,kuinua, kushawishi,kuboresha hali na ustawi
wa kiuchumi na jamii ya wanachama wake.
“mtandao huu utakuwa
ni kiungo kati ya vikundi vipya na vya zamani ili waweze kuboresha shughuli zao
za ujasiliamali,kujenga uwezo wa elimu ya ujasiliamali kwa wanachama, kujenga
sekta binafsi na za serikali” alisema Lezile
Aliongeza kuwa vikundi
vya ujasiliamali ni vizuri sana kwasababu hata mashirika, serikali, na
wafadhili huangalia sehemu za namna hiyo katika kutoa mitaji na sio kwa mtu
moja mmoja.
Vikundi vingi vimekua
vikiishia njiani kutokana na wajasiliamalin wengi kutokuwa na elimu ya kutosha
ya kuendeleza mitaji yao kwenye biasha kwasababu kila biashara lazima kuwepo na
elimu juu ya uendeshwaji wa biashara hiyo.
kutoaminiana kati ya
wanavikundi kutokana na wachache kujiona kama kikundi ni halali yao na kutaka
kujimilikisha, kwakutokuwa na uaminifu, pia kushindwa kusimamia vizuri miladi
yao hata kama wanamtaji wa kutosha.
Elimu nyingi tumeona
zinatangazwa juu ya elimu ya ujasiliama kutokana na kuamini kuwa mjasiliamali
hataweza kuendesha biashara yake asipo kuwa na elimu itakayo mwezesha katika
kufanikisha lengo lake
Suala la ajira kwa
nchi yetu ni tatizo kubwa hasa vijana wanaomaliza elimu zao wakitegemea kupata
ajira serikalini au katika mashirika mbalimbali na hatimaye kujikuta
wakizunguka na bahasha miaka mingi bila mafanikio.
Vijana mara nyingi
wanailaumu serikali kwa kushindwa kutengeneza mifereji ya ajira kwao, huku
serikali kupitia wizara ya ajira ikitoa majibu kadha wa kadha.
Njia pekee ambayo
vijana wanahashwa kufanya katka kutekeleza malengo yao ni kujiajiri kutoikana
na elimu ya ujasiliamali wanayoipata na sio kutegemea kuajiriwa.
Japo ushauri huo
vijana hawaukubali kwasababu ya kudai watajiajiri vipi wakati hawana mitaji?,
serikiali haiwapi nafasi, vijana hawaaminiki na hata hivyo vijana
hawathaminiwei katika taifa lao.
Licha ya faida zote
hizo juu ya elimu ya ujasiliamali hukisaidia kikundi cha URICO kuwa wabunifu
katika kuanzisha biashara mpya maeneo ambayo bado bidhaa zao hazijafika na
tayari kuna wateja.
Mipango ya biasha kwa
siku za usoni ili kupanua soko lao na kuweza kupambana katika soko la biashara
kwa kuwafikia wateja walipo na kutoa huduma nzuri na safi ili kuweza kuongeza
uaminifu wao na kushinda ushindani juu ya vikundi vingine.
Mtaji ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia katika kuzalisha
kitu kingine kwa lengo la kupata faida,biashara yoyote lazima ianze na mtaji.
Mtaji wa fedha au yeye mwenyewe mjasiliamali anaweza kuwa mtaji mfano kwa
ujuzi, elimu na kufanya kazi kwa bidii.
Wajasiliamali wengi wanapata changamoto kubwa katika kupata
mitaji ya kuanzishia biashara. Ni vigumu kuanzisha biashara bila kuwa na mtaji
wa kutosha,hivyo basi mtaji ni muhimu sana lakini mtaji pekee hautoshi
kuanzisha biashara.
Ni lazima uwe na elimu ya ujasiliamali ili uweze kufanikiwa
katika biashara. kuna njia mbalimbali za kupata mtaji na njia hizo ambayo ni
vyanzo vya ndani au vyanzo vya nje mfano Mtaji toka kwa
mjasiliamali mwenyewe.
Huu ni mtaji ambao mjasiliamali anakuwanao kabla hajaanza
biashara. huu ni mtaji bora sana kwani humilikiwa na mjasiliamali mwenyewe na
hatakiwi kurudisha rejesho hata baada ya kupata faida.
Pia Mtaji ambao
unapatikana wakati biashara inajiendesha ni faida inayopatikana katika biashara
inaweza kutumika kama mtaji,njia hii ndio huchangia kukua kwa biashara.
Mkopo toka benki, huu
ni mkopo ambao ulipaji wake ni wa muda mrefu,viwango vya riba si vikubwa sana
ambavyo mjasiliamali anaweza kumudu kulipa endapo biashara itafanikiwa, mikopo
ya benki inahitaji dhamana ya vitu visivyo hamishika mfano nyumba, shamba nk.
Nawakumbusha tu, yawezekana mlijisahau
Post a Comment