PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: NGO's YA FOUNDATION FOR TOMMOROW YAZINDUA KAMPENI YA SHAMIRI ILI KUSOMESHA WATOTO WA MITAANI 112 JIJINI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Meneja Mahusiano shirika  la The Foundation For Tommorow ,Anton Asukile akifafanua jambo juu ya Kampeni ya SHAMIRI inayolenga kuchangish...
Meneja Mahusiano shirika  la The Foundation For Tommorow ,Anton
Asukile akifafanua jambo juu ya Kampeni ya SHAMIRI inayolenga
kuchangisha milioni 50 kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi kwenye
mazingira hatarishi ,kulia ni Meneja Programu wa masuala ya kijamii na
afya Hedwiga na kushoto ni  Hilda Lema (Mfanyakazi).Picha na Ferdinand shayo



Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Tommorow limezindua
 kampeni  ya kuchangia  SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi
kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha  kiasi cha shilingi
milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na
mazingira yanayowakabili.

Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile alisema hayo jana
akizindua  kampeni  maalumu ya SHAMIRI   inalenga  kusaidia ustawi wa
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

“Kampeni hii itawezesha kuinua uchumi wa kaya 40  za watoto  wanaoishi
katika mazingira hatarishi  kupitia mradi wa WEZESHA KAYA pia
itasaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia kwa watoto
wapatao 112” Alisema Anton

Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki  katika kukabiliana na
changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto wanoishi katika
mazingira hatarishi kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.

Alisema kuwa Watanzania wataweza kuchangia fedha hizo kwa njia ya simu
katika  kampeni hiyo imeanza rasmi mwenzi Julai na itahitimishwa
septemba 25 mwaka huu.

Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga amesema kuwa
baada ya kutoa misaada kwenye familia duni wameona ni vyema
wakazipatia mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili waweze kujikwamua na
kusomesha watoto wao pasipo kutegemea misaada.
Hedwiga ameitaka jamii ya watanzania kuamka na kusaidia watoto yatimana wanaotoka kwenye familia masikini badala ya kusubiri mashirikakutoka nje yaje kutoa misaada.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top