NGO's YA FOUNDATION FOR TOMMOROW YAZINDUA KAMPENI YA SHAMIRI ILI KUSOMESHA WATOTO WA MITAANI 112 JIJINI ARUSHA
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Tommorow limezindua
kampeni ya kuchangia SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi
kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha kiasi cha shilingi
milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na
mazingira yanayowakabili.
Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile alisema hayo jana
akizindua kampeni maalumu ya SHAMIRI inalenga kusaidia ustawi wa
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
“Kampeni hii itawezesha kuinua uchumi wa kaya 40 za watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi kupitia mradi wa WEZESHA KAYA pia
itasaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia kwa watoto
wapatao 112” Alisema Anton
Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki katika kukabiliana na
changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto wanoishi katika
mazingira hatarishi kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.
Alisema kuwa Watanzania wataweza kuchangia fedha hizo kwa njia ya simu
katika kampeni hiyo imeanza rasmi mwenzi Julai na itahitimishwa
septemba 25 mwaka huu.
Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga amesema kuwa
baada ya kutoa misaada kwenye familia duni wameona ni vyema
wakazipatia mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili waweze kujikwamua na
kusomesha watoto wao pasipo kutegemea misaada. Hedwiga ameitaka jamii ya watanzania kuamka na kusaidia watoto yatimana wanaotoka kwenye familia masikini badala ya kusubiri mashirikakutoka nje yaje kutoa misaada.
Post a Comment