Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga(Shinyanga Press Club- SPC) |
Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga David Nkulila akizungumza jambo wakati wa uchaguzi leo mjini Shinyanga
Kulia ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake Shija Felician akimpongeza mwenyekiti mpya wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Kadama Malunde(aliyevaa suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi leo
Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde,ambaye ni mkurugezi wa Malunde1 blog akiwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician
Viongozi wapya wa SPC wakiwa meza kuu
Katibu mkuu mpya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Stephen Wang'anyi akizungumza baada ya uchaguzi,kushoto ni mweka hazina aliyetetea kiti chake bi Stella Ibengwe
Baadhi ya viongozi wa SPC wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
CHAMA
cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC)
jana Julai 23, 2015 kimefanya Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi
watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo
ambapo mwanahabari, Kadama Malunde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa
chama hicho.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi
wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila
alisema, Malunde ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea
wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.
Kadama
Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na
Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha
Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN).
Nkulila
aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa ni Stephen
Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa Makamu
Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella
Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.
Baada
ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo,
kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala yake
kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na
mabadiliko katika klabu hiyo.
Akizungumza mara
baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, Kadama aliwashukuru
wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze kushirikiana nao
kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari mkoani hapo pamoja na
kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi kutenda haki kwa kila
mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wa kazi za chama.
Post a Comment