PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: NYALANDU APOKEWA NA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA NA KUSEMA HIZI NI ZAMA ZA VIJANA KUSHIKA MADARAKA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
   Pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwa na Mkewe Faraja Kota wakiwa wanasalimia mamia ya watu wali...
 
 Pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwa na Mkewe Faraja Kota wakiwa wanasalimia mamia ya watu waliojitokeza ofisi ya CCM wilaya ya Arusha kumdhamini jana ambapo aliwashukuru na kuwataka kumuunga mkono safari ya Ikulu.


Mussa Juma.
Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu, ambaye anaomba kuteuliwa na chama cha Mapinduzi(CCM) kugombea Urais, jana alitua jijini Arusha kusaka wadhamini, huku akisema hizi ni zama za vijana kutawala.
Akizungumza na mamia ya wakazi wa jiji la Arusha, katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Arusha, Nyalandu alisema, kila zama ina uongozi wake na safari hii ni zama za vijana.
"nimetembea mikoa yote, nimeona shauku ya vijana na hii ni fursa yao kushiriki kulijenga taifa hili na kwa kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini"alisema

Hata hivyo, alisema chama cha mapinduzi(CCM), kina wakati mgumu kupitisha mgombea wake, kwani wagombea wengi waliojitokeza wanasifa lakini anatakiwa kiongozi ambaye anawaunganisha wanachama wote wa CCM.
"tunapaswa kuwa na kiongozi ambaye ataendelea kuwaunganisha watanzania wote bila kujali, dini zao, kabila wala rangi"alisema Nyalandu.
Alisema amefanikiwa kufika mikoa yote ya Tanzania na atahitimisha zoezi la kusaka wadhamini katika mkoa wake wa Singida na kote alipopita amejionea jinsi watanzania walivyo na imani na CCM.
"mimi sisemi lazima niwe mimi na huu ndio ubinaadamu kwani hakuna ambaye anajua mambo yaliyojificha zaidi ya mungu"alisema
Alisema yeye anaamini ndani ya CCM kuna viongozi wengi wenye busara ambao wataweza kuteua mgombea ambaye ataendelea kazi nzuri iliyofanywab na viongozi waliotangulia ikiwepo kuwaunganisha watanzania wote.
"mimi nimejifunza mengi kwa marais wastaafu kuanzia Mzee Mwinyi, Benjamin Mkapa na sasa kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ameniteua kuwa waziri wake naona naweza kuendeleza kazi yao nzuri"alisema
Awali Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Feruz Bano aliwashukuru mamia ya wanaccm ambao wanaendelea kujitokeza kuwadhamini wagombea wa Urais ndani ya CCM ambao wanafika katika jiji la Arusha.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha,Dk Wilfred Soileli alisema Arusha ni jiji shwari na hakuna mgombea ambaye anaweza kufika na akakosa kupata wanaccm wa kumdhamini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top