PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BANKI YA POSTA YAZINDUA HUDUMA MAALUMU YA AKAUNTI KWA VIKUNDI VISIVYO RASMI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEC), Beng’I Issa, (kushoto), ak...

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEC), Beng’I Issa, (kushoto), akikata utepe kuzindua huduma maalum ya akaunti ya vikundi visivyo rasmi, jana.
KATIKA  jitihada za kuwafikia Watanzania mbalimbali Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua akaunti maalum kwa ajili ya Vikundi Visivyo Rasmi. Uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mtendaji  wa Shirika la Uwezeshaji Tanzania, Beng’I Issa katika viwanja vya Shule ya Msingi Osterbay, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema, sasa makundi mbalimbali yasiyo rasmi yanaweza kufungua akaunti na Benki ya Posta na kuweza kupatiwa mikopo ya riba nafuu ya kuwawezesha katisha shughuli zao za ujasiriamali. 
‘Tunaposema akaunti za vikundi visivyo rasmi, ni vikundi kama vile jogging, vilabu mbalimbali vya michezo, wasuka nywele, wasuka mikeka n.k., aliongeza Moshingi.

Makundi mengi yamejitokeza katika kufungua akaunti hizi za vikundi visivyo rasmi, na hadi sasa akaunti takribani 340 zimefungulia kwa makundi yasiyo rasmi, alisema Moshingi. Kwa wiki benki inafungua akaunti zaidi ya 16 kwa makundi haya, na tunapenda kuwahamasisha makundi haya yajitokeze kwa wingi, ili waweze kunufaika na akaunti hii, alisema Moshingi.

Kwa upande wake Beng’i Issa, alitoa pongezi kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kubuni akaunti hiyo maalum kwa makundi hayo. ‘Makundi mengi yanatamani sana, kupata huduma za kibenki kwa ajili ya shughuli zao za kila siku, ila kutokana na uwezo sababu zilizo nje ya uwezo wao wanashindwa kupata huduma hizo’, alisema Issa. Sasa makundi haya yajitokeze kwa wingi katika kufungua akaunti hii Benki ya Posta iliwaweze kupata huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo, mikopo n.k aliongeza Issa.

Benki ya Posta Tanzania ni miongoni mwa mabenki yanayokuwa kwa kasi nchini, ikifuata sera ya financial inclusion, yaani kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za kifedha hapa nchini. 
Benki hii hivi sasa ipo katika mchakato wa kubadilisha sharia iliyoanzisha Benki ya Posta Tanzania, Sura ya 301, ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha na kanuni zake (The Banking and Financial Institution Act, 2006 and its Regulations), ambayo imeweka masharti kwa benki zote nchini kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni, sura 212. Mchakato huu wa kubadilisha sharia hiyo uko Bungeni hivi sasa na uko katika hatua nzuri, na unalenga kuiwezesha Benki ya Posta Tanzania kukidhi matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha na Kanuni zake. 
Akizungumza mchakato huu, Moshingi alisema mara baada ya kukamilika kwake, benki yake itaweza kujiimarisha zaidi na kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake, katika wigo mpana zaidi.
 Wajasiriamali, wakiwa wamekamata kadi ya ATM ya benki ya Posta, baada ya benki hiyo kuzindua, huduma ya akaunti maalum kwa vikundi visivyo rasmi, jijini Dar es Salaam


 Katibu Mtendaji wa NEC, akizungumza wakayi wa uzinduzi huo
Maafisa wa juu wa benki hiyo, wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top