Wakazi wa kata ya Sinoni wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kupiga kura,vituo vinakabiliwa na idadi kubwa ya watu ukilinganisha na uchache wa mashine za BVR .Picha na Ferdinand Shayo |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Zoezi la Uandikishaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa
mfumo wa kisasa wa BVR umechukua sura mpya kutokana na baadhi ya watu kuwauzia watu nafasi za kuingia katika vituo
vya kujiandikishia hivyo kugeuka
biashara kwa wanaokwepa foleni ndefu na
kukesha katika vituo.
Wananchi wa
Kata ya Sinoni jijini hapa Hussein Issa na
Swalehe Ramadhani wameeleza kuwepo kwa baadhi ya vijana ambao wamekwisha
kujiandikisha lakini hufika kituoni hapo na kushika nafasi za mbele ambazo
wanawauzia watu wengine mchezo ambao umekithiri katika vituo vingi.
Issa alisema
kuwa nafasi moja huuzwa kati ya shilingi 15000 hadi 10000 kwa mtu mmoja nafasi hizo hugombaniwa na watu wengi .
“Watu wamegeuza BVR kama biashara wanashika nafasi
na kuwauzia watu jambo ambalo linakwamisha zoezi wengi wasiokuwa na kitu cha
kutoa wanakaa kwenye foleni kwa muda mrefu bila mafanikio” Alisema Issa
Polpodia
Massawe mkazi wa Esso analalamikia mfumo huo kuwa bado haujaweza kukidhi idadi
kubwa ya watu kwani imemlazimu kuacha shughuli za kujiingizia kipato na kupanga
foleni kwa muda wa siku 4 bila mafanikio.
Aliasema
kuwa watu wengine wamekua wakikesha na kulala vituoni hapo ili kuwahi nafasi
hadi kinamama wenye watoto wadogo hivyo ameitaka serikali iongeze nguvu hasa
kwenye vituo vya mijini vyenye idadi kubwa ya watu.
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Daudi Filex Ntibenda aliyetembelea kituo hicho amekaripia vikali
tabia ya watu kuuza nafasi maarufu kama ploti kwani ni kinyume cha utaratibu
pia amewataka wanasiasa kutoingilia suala la uandikishaji na kuishia
kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi.
Post a Comment