Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Waislamu kote nchini wametakiwa
kujiandaa vyema na mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajia kuanza hivi karibuni
kwani kipindi hicho ni cha kufanya matendo mema na kuisaidia jamii hasa
wahitaji .
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa taasisi ya Islamic
Foundation Bader Marei jana
katika swala ya ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Alsahaba
ulioko eneo la kwa Morombo jijini hapa na kuhudhiriwa na Balozi wa falme la
kiarabu nchini .
Bader huyo amesema kuwa kipindi
cha Ramadhani ni kipindi cha kujitazama na kubadili mwenendo na
kuwa watu wanaofaa katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Ugeni huo wa
Ubalozi wa falme hizo za kiarabu amesema kuwa ziara hiyo inalenga kuangalia
changamoto za kijamii na kuangalia namna ya kuzitatua ambapo wamezindua visima
34 vya maji katika wilaya ya Ngorongoro.
Mbali na shughuli hizo pia wamegawa
msaada wa tende kwa waislamu wote waliohudhuria katika swala hiyo ikiwa ni moja
kati ya maandalizi ya Mwenzi huo mtukukufu.
Baadhi ya waumini walioshiriki katika
swala hiyo Issa Tesha muuminI na Saidi Hamis
muumini wameeleza kufurahishwa na ujio huo mkubwa ambao unashirikiana na
jamii ya waislamu katika masuala mbali mbali ya kijamii na kidini.
“Tumefurahi kupata msaada
wa tende kipindi cha Ramadhani upatikanaji wa tende huwa mgumu lakini sasa
walau tuna tende tunashukuru sana “ Alisema Issa
Post a Comment