Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akisamilia na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Meng
MWENYEKITI wa makampuni ya IPP, Regnald Mengi ameendelea kung’ang’ania
kuwa, kauli zinazotoka Ofisi ya Rais Ikulu, zinazidi kumpa wasiwasi na
hofu kubwa katika maisha yake.
Mengi ameeleza wasiwasi huo leo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake, na kueleza masikitiko yake juu ya kauli za dharau na dhihaka zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Salva Rweyemamu.
Mengi amesema kuwa, Aprili 17 mwaka huu, alizungumza na waandishi juu ya
hofu yake, baada ya kupata habari kutoka kwenye gazeti la Taifa Imara
la Machi 23 mwaka huu.
Habari hiyo iliosema, “Zitto Kabwe amchongea Mengi kwa Kikwete kwamba ndiye kinara wa kuihujumu Serikali yake.”
Mengi ameongeza “habari hiyo iliendelea kusema kwamba, nimeapa
kumshuhgulikia Rais Jakaya Kikwete kwa nguvu zangu zote amalizapo muda
wake wa urais, na kwamba Rais aliapa kupambana na mimi.
Amesema kauli hizo dhidi yake zilimshtua sana, na kwamba yeye hakuzitoa,
hivyo kauli ya Kikwete ya kutaka kupamba naye ilizidi kumpa hofu ya
usalama wa maisha yake.
“Kutokana na mwingiliano wa kauli hizo, pia nililaumu sana Kurugenzi ya
Mawasiliano- Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa kukaa kimya zaidi ya
wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote katika jambo hili linalomhusu Rais
na kuacha habari hizo kusambaa,” ameeleza Mengi.
Amedai kuwa, katika majibu ya Rweyemamu, alisema “Rais hakuwahi kuwa na mawasiliano yoyote na Zitto Kabwe kama ilivyoelezwa.”
“Hivyo, katika majibu yake Rweyemamu, alidai kuwa, hakufanya lolote eti
kutokana na kuwa na majukumu mengi na alipuuza habari hizo kwa sababu
aliziona ni jambo dogo na ni la upuuzi,” ameeleza Mengi.
Kwamba Rweyemamu kwa jeuri, aliongeza kuwa, alimshangaa sana kwa
kutokutoa taarifa latika kituo chochote cha polisi kuhusu hofu ya maisha
yake.
“Kauli hizo, zinaongeza hofu ya usalama wa maisha yangu. Jambo hilo sio
dogo la kupuuzwa kama linavyodaiwa. Rweyemamu hakutumia busara katika
majibu yake, kutokana na kiti chake na heshima aliyonayo, alipaswa kutoa
kauli nzuri na sio kuzidi kunipa hofu.
“Na kwa upande wa Rais, mimi sina ugomvi naye na ninaamini yeye pia hana
tatizo na mimi ila kauli za huyo mtu ndizo zinanipa shida,” amesema
Post a Comment