Na Ferdinand Shayo,Arusha.
WAFUGAJI kutoka Wilaya za Ngorongoro ,Longido na Monduli
wameeleza kuanza kukumbwa na athari za matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa na
tabia nchi.
Wakizungumza katika kongamano la jamii za kifugaji
zinazoishi katika nyanda kame lililoandaliwa na shirika la Haki
kazi Catalyst na taasisi ya kimataifa ya mazingira na
maendeleo (IIED) viongozi wa jamii hiyo walisema kuwa tayari
wameanza kukosa mvua za kutosha katika maeneo yao
“ Joto limekuwa kali sana, mvua hazitabiriki ,tunashindwa kujua
misimu tuliyozea,wakati mwingine mvua kubwa inanyesha kiasi cha kuleta hofu na
mafuriko makubwa tofauti na siku za nyuma ,hali hii ni ishara kuwa hali
ya siku zijazo ni tete”alisema Martalo.
Diwani
wa viti maalum kutoka Wilaya ya Ngorongoro Tina Timan alisema kuwa kwa
sasa wanawake wa jamii hizo wanasafiri umbali kutafuta maji kufuatia vyanzo vya
maji kukauka kufuatia hali ya ukame.
“Nimefurahi
kwa mpango huu na hasa kutokana na kushirikisha wanawake wa jamii za kifugaji
ambao ndio wahanga wakubwa wa tatizo hili ,sisi ndio tunasafiri mbali kufuata
maji ,kutafuta kuni ” .anasema Tin
.
Tina
aliongeza kuwa migogoro ya ardhi na sera mbalimbali zinawaweka wafugaji katika
hatari zaidi ,maeneo yao yanachukuliwa na kugeuzwa hifadhi na mengine kupewa
wawekezaji tunaomba katika mikakati hii hili nalo litazamwe.
Esupat
Ngulupa kutoka Longido alisema kuwa miaka michache iliyopita wafugaji
walipoteza idadi kubwa ya mifugo baada Wilaya hiyo kukumbwa na ukame
uliodumu kwa muda mrefu.
“Tunashukuru
mashirika haya kujitokeza kutuelimisha namna ya kupambana athari zitokanazo na
mbadiloko ya hali ya hewa na tabia nchi”alisema Esupat.
Kwa
upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka taasisi ya kimataifa
ya mazingira na maendeleo (IIED)Alais Morindat alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia jamii hiyo kuweka mikakati
na mipango ya kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi.
“Kila Wilaya ina mratibu
ambaye pamoja na wawakilishi wa jamii katika Wilaya husika wataweka mipango ya
kukabiliana na matokeo ya tatizo hili’alisema Morindat.,
Alisema kuwa jamii pamoja
na viongozi wa kisiasa ilishiriki kikamilifu katika kongamano hilo na
kutoa mawazo na uzoefu, kutafakari kwa pamoja sera na
dira ya maendeleo ya taifa katika kuondoa umaskini na jitihada za taifa katika
kukabili mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
Aidha Morindat aliongeza kuwa washiriki
pia walijadili kwa undani masuala ya msingi juu ya dhana na
Sayansi ya mabdiliko ya hali ya hewa na tabia Nchi pamoja
na Mifumo ya wafugaji iliyopo na inayopotea katika kuhimili
mabadiliko mbalimbali yanayotokea.
Sera na sheria
za nchi na jinsi inavyowezesha ama kutowezesha mifumo hiyo ya kijamii kufanya
kazi na mabadiliko makubwa ya kiuchumi duniani faida na athari zake kwa mifumo
ya Kijamii.
Post a Comment