PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA YA UCHUMI-JIFUNZE KUONA FURSA AMBAZO WENGINE HAWAZIONI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Shayo. Fursa ni nafasi ambazo zinaweza kumwingizia kipato mtu na kama zitatumika vizuri ...




Na Ferdinand Shayo,Shayo.

Fursa ni nafasi ambazo zinaweza kumwingizia kipato mtu na kama zitatumika vizuri na kwa wakati unaofaa zinaweza kubadilisha  kabisa maisha yako.
Ili kuona fursa hauhitaji kuwa na mabilioni bali unachohitaji ni kuwa na macho ya kuona na kutambua fursa ambazo wengine hawazioni.
Katika mazingira tunayoishi  yamejaa fursa nyingi ambazo  zipo hapo hapo ulipo ,wakati unayalaumu mazingira kuna watu wanatajirikia kwenye mazingira hayo hayo ,hapo utagundua kuwa tatizo sio mazingira tatizo  ni macho ya kuona fursa.
Macho ya watu wengi huelekea kwenye vitu vilivyotayari  kwasababu ya uvivu wa kufikiri hawapendi kusumbua akili zao kuvifanya vile visivyoonekana vionekane kwa maana ya kuvumbua vitu vipya  na kubaki kugombania vile vinavyoonekana.
“Mtu mwenye uwezo mzuri wa kuona ni Yule anayeona vitu ambavyo wengine hawavioni  hata kama wanayo macho ya kuona” kinaeleza kitabu cha cha Maarifa “Chochote kinaweza kuwa kama Dhahabu” kilichoandikwa na  Lion Mangole .
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kuwa “What you see what you get” akimaanisha kuwa unachokiona ndio unachokipata.
Ukiwauliza watu wengi wanaona nini katika mazingira yao wanakwambia wanaona shida,mazingira mabovu ,unakutana na mtu mmoja akimuuliza anakuambia anaona fursa ya kuanzisha biashara,kampuni,taasisi.
Eneo ni moja ila macho yanayotazama ni tofauti mmoja anaona fursa wengine wanaona matatizo ndio maana kuna gepu ya kiuchumi kati ya mtu na mtu ,na gepu hiyo haitakwisha kama macho yao yataendelea kuona kiutofauti.
Kuwa na macho yanayoona fursa za kibiashara,kiuchumi ni muhimu kwa kila mtu anayehitaji fedha hapa duniani.
Ni ukweli usiopingika kuwa mfumo uliopo hapa duniani ili upate mahitaji muhimu ni lazima uwe na fedha .
Fedha inapatikana kwa nguvu ya mbadilishano  (power of exchange) ili upate fedha lazima uwe na kitu cha kubadilishana na fedha  aidhaa bidhaa kwa fedha ama huduma kwa fedha.
Mazingira haya haya tunayoyaona mabovu  hayafai wako wachache wanaoyatumia kuanzisha biashara,taasisi na kufanikiwa ile hali wengi wakibaki kulalamika.
Mtaalamu mmoja wa masuala ya uchumi nchini alikua akienda uwanja wa ndege kusafiri ughaibuni alikutana na vijana kadhaa na wao wakihitaji kuruka na ndege kwenda nchi za nje alipowauliza maudhui ya safari yao wanakwenda kutafuta maisha kwa maana ya fursa za kiuchumi ,aliwashangaa kwani wakati huo kuna wageni kutoka nje wanakimbilia kuja nchini kutumia fursa ambazo wenyeji hawazioni.
Bila kuwa na macho ya kuona fursa za kiuchumi ni vigumu kufanikiwa ,tatizo sio kuhama sehemu moja kwenda nyingine kikubwa ni nini unakiona katika mazingira uliyoko.
Unapokuwa na macho ya kuangalia fursa utagundua kuwa hapo ulipo unatembea kwenye mawe ya  dhahabu hivyo huna haja ya kwenda sehemu nyingine kutafuta dhahabu.
Tusibaki na wimbo wa kusema kuwa Watanzania ni masikini na kuanza kutafuta nani mchawi aliyewaloga watanzania .
Kumbe tatizo ni macho ya watanzania wanatakiwa waamke wafungue macho na akili zao ili waweze kuona kuona fursa zilizopo kwenye mazingira yao badala ya kuyalalamikia.
“Kufungua macho sio kuamka” Nukuu ya Msanii Fareed Kubanda wa Mwanza .Wako waliofungua macho wakaziona fursa lakini bado wamelala hawajaamka  kwa maana ya kuchukua hatua na kuzitumia fursa hizo ili ziweze kubadilisha maisha yao.
Fursa za kibiashara zinaweza kutokana na mahitaji ya watu.Tunapoaangalia mahitaji ya watu na kugeuza kama fursa ya biashara, basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini vile vile tutakuwa tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla, kwa kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi chakula,maji,usafiri. itashangaza kusikia kwamba hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka.

0765938008

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top