Mratibu
wa shughuli za ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Bw. Senya Tuni (Wapili
kulia) akieleza jambo mara walipoingia kwenye eneo la gati la Bandari ya
Mbaba Bay. Wanaomsikiliza ni Mkuu wa msafara huo, Bibi Florence Mwanri
(Kulia), Afisa mazingira wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Julius
Edward (Watatu kulia). Na kushoto ni Bw. Jordan Matonya ambae ni Mchumi
kutoka Tume ya Mipango.
Baadhi ya wajumbe wa timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakiingia kwenye gati la Bandari ya Mbaba Bay iliyopo wilayani Nyasa
mkoani Ruvuma.
Afisa
bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio (Wapili kushoto) akitoa maelezo
kwa wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango walipofanya ziara kwenye bandari hiyo. Timu hiyo iliongozwa na
Bibi Florence Mwanri (Kushoto).
Kiongozi wa timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence kushoto akionesha kitu kwenye sehemu ya gati la
Bandari ya Mbaba Bay (halionekani).
Baadhi
ya utajiri unaopatikana kwenye Ziwa Nyasa. Dagaa wa Ziwa hili ni
maarufu kwa utajiri wake wa lishe. Kwa mujibu wa wakazi wa Mbaba Bay,
dagaa hao uuzwa hadi nje ya nchi.
*******************************************************
Timu
wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango
imetembelea Bandari ya kimkakati ya Mbaba Bay iliyopo wilaya ya Nyasa
mkoani Ruvuma kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bandari hiyo.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
alisema kwamba Bandari hiyo ni muhimu kwa uchumi wa nchi kwa kuzingatia
eneo la kijiografia la bandari hiyo.
“Bandari
hii ni muhimu kwani kijiografia inaweza kuzifikia nchini nyingi zilizo
kusini mwa nchi yetu hivyo inaweza kutumika kama lango la kibiashara
miongoni mwa jirani zetu licha ya uhaba wa miundombinu yake,” alisema.
Aliwasihi
wafanyakazi wanaoihudumia Bandari hiyo kufanya kazi kwa bidii bila ya
kuchoka ili kuweza kuvutia wafanyabiashara na watumiaji wengine
kuendelea kuitumia bandari hiyo.
Kwa
upande wake, afisa bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio aliutaarifu
ugeni huo kuwa Mamlaka ya Bandari ipo katika mkakati wa kuindeleza
bandari hiyo ili kuweza kuihudumia wateja wengi zaidi.
Pia, Bw. Urio aliwashukuru wajumbe wa timu hiyo ya ukaguzi kwa kwenda kuitembelea na kujionea maendeleo ya bandari hiyo.
“Tunafarijika
sana kuona viongozi wa serikali wanapokuja kututembelea kwani hali hii
uongeza hamasa ya utendaji kazi wetu,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016)
bandari ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.
Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo
lengo kuu likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo
ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje ya nchi;
Maendeleo ya viwanda: Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na
kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama
vile viwanda vya nguo, mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za
chuma) na pia sekta ya madini kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.
Pamoja
na kipaumbele cha Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi: Mpango
unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya
ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma)
katika kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na
kijamii; na Utalii, Biashara, na huduma za Fedha ambapo jitihada
zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa kuuza katika masoko ya ndani na
nje, kuongeza idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na
kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha.
Post a Comment