Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, akizungumza wakati akiifungua semina ya Kujadili masuala ya Uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa jamii nchini, Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyoandaliwa na wizara hiyo, imefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) |
Mwakilishi Mkazi wa ADB, Tonia Kandiero wakati semina ya
Kujadili masuala ya Uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa jamii
nchini, Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyoandaliwa na wizara hiyo,
imefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB).
Baadhi ya wadau wa semina hiyo .
Naibu
Waziri wa Fedha, Adam Malima, akizungumza wakati akiifungua semina ya
Kujadili masuala ya Uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa jamii
nchini, Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyoandaliwa na wizara hiyo,
imefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB).
Na Magreth Kinabo, MAELEZO
TANZANIA imepata alama ya pointi tano katika masuala ya uongozi bora kwenye ripoti ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika(Afrika For Results) ya mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na Waziri wa fedha,Adam Malima wakati akizungumza katika ufunguzi wa semina ya siku nne wa kutathimini ripoti hiyo kwa nchi ya Tanzania ukilinganisha na tafiti za nchi zingine za Afrika unaoendelea kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dares Salaam.
“ Katika ripoti hii kipimo cha alama zilizotumika ni 0-5 , hivyo Tanzania imefanya vizuri katika masuala ya uongozi bora kwa kupata alama hiyo,” alisema Malima .
Katika
ripoti iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika(ABD) ikishirikiana
na Serikali ya Tanzania ambayo imetaja maeneo sita ya kuzingatia katika
kuhakikisha ukuaji wa uchumi unafika kwa wananchi wote wakiwemo wa kawaida kwa kuzingatia hilo na mengineo.
Aliyataja maeneo hayo ambayo ni uwajibikaji kwa alama 4.1. uwezo wa kitaasisi alama 4, mikakati ya kibajeti alama 2.9, mipango yenye kuleta matokeo alama 4.5 na matumizi ya Tehama alama 2.3.
Naibu Waziri huyo alisema ili kutengeneza fursa sawa katika ukuaji wa uchumi ni muhimu kuboresha viashiria vya kukua kwa uchumi na kupunguza umaskini.
“Wananchi wa kawaida wanaambiwa kuwa uchumi umepanda kwa asilimia saba lakini, baadhi yao hali yao kimaisha bado ni duni na wanashindwa kuamini ukuaji huo hivyo kwa
kutumia viashilia hivyo tunaweza kugundua na kuboresha baadhi ya maeneo
ambayo yameonekana kuwa chanzo cha kutowafikia wananchi wa
kawaida,”alisema Malima.
Wadau hao katika mkutano huo watajadili njia
ambazo zitakazo saidia kuwafikia wananchi wa kawaida kukua kiuchumi ili
kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 ya kuwa nchi yenye
uchumi wa kati.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa ADB, Tonia Kandiero alisema wadau hao watajadili ripoti hiyo katika mkutano huo wa kutathimini ripoti hiyo kwa nchi ya Tanzania kwa siku nne , na kulinganisha na nchi zingine za Afrika unaoendelea kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dares Salaam.
Akitoa uzoefu wake katika nchi ya Zimbabwe, Erick Zinyengere,
ambaye ni Meneja wa Ushauri alisema ili kuweza kuleta mafanikio ya
kimaendeleo katika miradi mbalimbali ni vema kushirikisha wananchi katika hatua ya kwanza hadi ya mwisho.
|
Post a Comment