PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAKULIMA WA KAHAWA WAPATA FAIDA KUBWA KWA KUUZA KAHAWA MBICHI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
KILIMANJARO viongozi wa vyama vya Ushirika hapa nchini wametakiwa kuthamini ununuzi wa kahawa iliyo safi na yenye ubora ambao unakubalika ka...




KILIMANJARO viongozi wa vyama vya Ushirika hapa nchini wametakiwa kuthamini ununuzi wa kahawa iliyo safi na yenye ubora ambao unakubalika katika masoko.




Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro, Kasya Kasya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi.




Alisema chama cha ushirika ni chombo cha kiuchumi, kinapaswa kufanya biashara na kama hawatathamini bidhaa inayouzwa katika masoko yetu, madhara yake makubwa ni kuendelea kupata hasara.




Amefafanua kuwa ili kahawa iweze kumwongezea thamani mkulima ni vyema viongozi waliopo katika chama kuhakikisha wanasimamia kikamilifu, ununuzi wa kahawa ambayo haijachanganywa kitu chochote.

Aidha alitoa rai kwa wakulima wa zao hilo kuona umuhimu wa kuandaa kahawa yenye ubora ambayo itawapatia faida kubwa na kuachana na tabia ya kuuuza kahawa mbichi.




Kwa upande wao wakulima wa kahawa walielezea sababu za kuuza kahawa mbichi, ambapo walisema kuwa wengi wao wamekuwa wakiuza kahawa mbichi ili kuongeza uzito kwani wanapouza kahawa ambayo imekauka inapunguza uzito.




Mmoja wa wakulima hao, Edith Moshi, alisema wakulima wamekuwa wakiwahisha kuuza kahawa mbichi, ili kuweza kujipatia fedha za kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto wao shule, huku wangine kwa ajili ya kujitibu.




Kwa upande wake Meneja mkuu wa KNCU, Honest Temba alisema kahawa inapokuwa na unyevunyevu, asilimia 13 hadi 19 wanajikuta wanapata hasara ya mabilioni ya fedha kutokana na ununuzi wa kahawa mbichi.




Temba amewataka viongozi walioko zamu kwenye vyama vya msingi, kuwa makaini na kazi zao wakati wanaponunua kahawa ili kuwepuka hasara

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top