PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAJAMBAZI YAPORA FEDHA NA KUUA NJE YA KIWANDA CHA BORA JIJINI DARESALAAM MAPEMA LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Polisi akiingia bora Baadhi ya Polisi wa doria ya Pikipiki wakiwa nje ya kiwanda cha Bora. ***** Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ...



Polisi akiingia bora
Baadhi ya Polisi wa doria ya Pikipiki wakiwa nje ya kiwanda cha Bora.
*****
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamepora begi linalodaiwa kuwa na fedha kisha kumpiga risasi ya shingo mwendesha boda boda na kupora pikipiki yake nje ya Kiwabnda cha Bora, barabara ya Njerere Dar es Salaam mchana huu.

 kwa mujibu wa mwandishi  aliyefika eneo la tukio na kukuta watu wakielezea tukio hilo na kulifananisha na la sinema kutokana na kile walichokiona.


"Tuliona mzee mmoja tunahisi ni mfakazi wa Bora, alifika na pikipiki hapa, wakati anataka kuingia ndani wakafika watu wengine wawili katika pikipiki na kuamuru kupewa begi lile na ghafla mwenda pikipiki akawa anawahoji inakuaje wanachukua begi hilo ndipo tukasikia mlio wa risasi na bodaboda yule akaanguka chini wakamsukuma na kuchukua pikipiki yake na kukimbia nayo," alisema shuhuda yule.


Polisi ilifika eneo la tukio huku wengine wakiendelea na msako mkali dhidi ya wahalifu hao wakutumia sihala huku hofu ya kijana yule wa boda boda kupoteza maisha ikiwa kubwa kutokana na eneo alilopigwa risasi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top