MAKALA YA UCHUMI: SARAFU MPYA ZA MIA 500 NA KUPOROMOKA KWA THAMANI YA SHILINGI
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Takribani wiki moja imepita tangu sarafu ya shilingi 500 zilipoingia kwenye mzunguko wa fedha na kuanza kutumika baada ya mchakato wa kubadilisha fedha hizo kutoka kwenye noti kwenda kwenye sarafu ulivyokamilishwa na Benki kuu ya Tanzania (BOT).
Sarafu hizo zimepokelewa kwa hisia tofauti mitaani kwa Watanzania walio wengi hata wengine wakizihusizihusisha na kuporomoka kwa kwa kasi kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
Baadhi ya wananchi wametoa maoni yao wakiwemo wafanyabiashara ambao tayari wameanza kutumia sarafu hiyo wameonyesha kuiridhia lakini wengine wamekua na fikra tofauti .
Mfanyabiashara Aisha Bakari anaeleza kuwa sarafu hiyo inaashiria kushuka kwa thamani ya shilingi hofu yake kubwa ni kutoweka kwa sarafu za shilingi 50,100 na 200 ambazo zitakua chini sana katika thamani kama ilivyokua kwa shilingi 5,10 na 20 .
Mkazi wa Arusha Ticter Abubakari anaeleza kwa mara ya kwanza alipoziona alifikiri sarafu ya shilingi 10 imerudi kutumika ,fedha ambazo zimepotea kwenye mzunguko wa fedha ziko kwa wanaolipwa mishahara kwenye salary slip kuna shilingi mpaka senti lakini ukija mtaani kununua vitu hakuna.
Mia tano za sarafu inaonyesha wazi ni jinsi gani fedha yetu imeshuka ukilinganisha na fedha za nchi nyingine fedha kubwa marekani ni noti ya dola 100 ukija Tanzania fedha kubwa ni shilingi 10,000 inafika 500 ya noti inakua sarafu ni picha inaonyesha rasmi afadhali tulipotoka kuliko tunapoelekea.
Ticter anaeleza kuwa licha ya uchumi wetu kukua ambako kunatokana na uwekezaji wa madini na gesi bado thamani ya shilingi inaenda ikipungua thamani.
" Noti inabeba sarafu nyingi na senti,uwezekano wa sarafu kubeba sarafu nyingi na senti nyingi ni mdogo mno ,sarafu ya mia 500 ni udhihirisho wa thamani ya shilingi kushuka" Anaeleza Abedi Mohamedi
Meneja wa kitengo cha Uchumi ,Benki kuu ya Tanzania tawi la Arusha,Dr.Wilfred Mbowe anaeleza kuwa mabadiliko ya noti ya shilingi 500 kwenda kwenye sarafu hayahusiani na kushuka kwa thamani ya shilingi kwani bado thamani yake iko pale pale.
Dr.Mbowe anasema kuwa baada ya kuona noti ya shilingi mia 500 inazunguka mara nyingi hivyo inaweza kuchakaa sana ndipo ukafikiwa uamuzi wa kutengeneza sarafu .
"Mfano tungetengeneza noti ya shilingi 20,000 au 50,000 hapo tungeweza kusema thamani ya hela imeshuka kwasababu utahitaji fedha nyingi kununua kitu kilekile" Anafafanua Mchumi huyo.
Mchumi huyo anaeleza kuwa fedha zinazozunguka mara nyingi huwa zinachakaa haraka kwa hizi shilingi 500 za noti tuliona zinazunguka sana na zinawahi kuchakaa zikaja hizi sarafu.
Kinachofanya hela ya thamani fulani iwepo kwenye mzunguko ni mahitaji ukiangalia shilingi 500 inanunua vitu vingi .
Uimara wa fedha unategemea na vitu vingi hela hela yake ina nguvu zaidi,ni pamoja na kuuza bidhaa nje ya nchi,kuingiza bidhaa ndani ya nchi,uzalishaji wa ndani.
Vile vile uimara wa fedha unapimwa pia kwa kulinganisha dhidi ya fedha nyingine.
Anaeleza kuwa fedha haiwezi kuwa imara kama nchi haizalishi vya kutosha,haiuzi bidhaa nje ya nchi na kudhibiti mfumuko wa bei.
Mabadiliko ya fedha unatokana na mabadiliko ya teknolojia wakati mwingine fedha zinabadilishwa ili kuendana na teknolijia,kuzuia uchapishaji wa fedha bandia ama hela inapopoteza thamani japo kwa Tanzania bado hela iko imara.
Hela zimekua zikibadilishwa mara kwa mara,miaka michache tulianzisha noti mpya ili kuzuia kufojiwa,kukidhi mahitaji ya makundi maalumu wasioona na kuhakikisha kuna fedha safi kwenye mfumo wa mzunguko wa fedha .
ferdinandshayo@gmail.com
0765938008
Post a Comment