Mwanaharakati
Peter Ahham anaeleza kuwa rasimu ya sita imekosa viwango vya ubora wa
kisiasa wa kimataifa ulioweka na Jumuiya
za Madola ambapo Tanzania ni mwanachama,Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na
Umoja wan chi za Afrika (AU) .
Viwango vya
ubora wa siasa kimatiafa vinaelekeza kujali mawazo mbadala na kujali upinzani
hali ni tofauti kwa Bunge la katiba.
Rasimu ya
Sita imekosa uhalali kutokana na kukosekana kwa ushiriki wa chama kikuu cha
upinzani pamoja na vyama vingine vya siasa.
Sio kwamba
kila kitu ni kibovu katika rasimu ya sita ila kuna vipengele Muhimu vya maslahi
ya taifa vimeondolewa mfano wabunge wawe
na ukomo na wawajibishwe .Vipengele hivyo vimeondolewa Mbunge anaweza
kulala mpaka muda wake ukaisha bila kuwajibishwa.
David
Mustapha ,mkazi wa Sombetini anaeleza kutokubaliana na rasimu hiyo kwa kuwa hata
Mwanasheria wa Zanzibar hajakubaliana nayo yeye kama Mwakilishi anayetegemewa
na Raisi wa Zanzibar na Wananchi kwa ujumla.
Mfumo wa
kupiga kura kwa mitandao ya kijamii ni ubatili kwasababu ni vigumu kuamini kuwa
anayepiga hiyo kura ndio mtu mwenyewe na wengine wana akaunti zaidi ya moja
hiyo wanaweza kuharibu mchakato a kupiga kura.
Mkazi wa
Ngaramtoni Joel Ndumbalo anaeleza kuwa maoni ya wananchi yamechakachuliwa kwa kiasi kikubwa na pia upande wa pili wa wapinzani
haujasikilizwa mapokezi yah ii rasimu
yatakua tofauti.
Mwambanga
Msigwa ,mkazi wa Sombetini anasema
kuwa Bunge la katiba limeenda
vizuri kuna vifungu ambavyo si
vizuri mfano kipengele cha Raisi wa
Zanzibar kuwa Makamu wa Kwanza wa Raisi
,kuna hatari ya kuwa na Raisi ambaye hatujamchagua kwasababu sisi hatumchagui
Raisi wa Zanzibar inapotokea dharura anashika madaraka kama Raisi kwa muda
Mwenyeji wa
Unguja ambaye ni Mkazi wa Arusha Omar Bashir anaeleza kutoikubali rasimu kwa
kuwa imeondoa maoni ya wananchi juu ya
kuwepo kwa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na wananchi pia kuifanya
Zanzibar iwe na heshima kama nchi.
.
Ticter
Abubakar anaeleza kuwa hata kabla ya kuangalia rasimu yenyewe mwenendo wa Bunge
la katiba ulikua hauridhishi malumbano na mada ziilizokua zikijadiliwa
hazimlengi Mtanzania bali zilijikia zaidi kwenye ustawi wa viongozi na maslahi
yao .
MKazi wa
Morombo ,Joseph Shenga afafanua kuwa kutokana na mwenendo wa Bunge hilo
matarajio ya wananchi kupata katiba bora yako chini baada ya kuona rasimu ya
warioba imepuuzwa kwa kiasi kikubwa.
Abdala
Omari ,Rasimu imepitishwa kibabe na kwa kulazimisha wamepindisha maoni ya wananchi yaliyopelewa
na warioba rasimu tunayokubaliana nayo ni ya warioba.
Post a Comment