Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Akifungua semina ya ujasiriamali mapema leo. picha na KEPHAS ILANI |
Mkurugenzi wa chuo chuo cha uandishi habari na utangazaji Arusha bwana Joseph Mayagila amefungua semina ya siku tatu ya ujasiriamali leo itakayomalizika siku ya ijumaa chuoni hapo.
Bwana Joseph Mayagila amesema kuwa semina hiyo ni muhimu
sana kwa wanafunzi wote kwa sababu dunia ya sasa imejengeka katika misingi ya
ujasiriamali.
Alisema kuwa ili mtu yeyote afanikiwe kibiashara ni lazima
ajue kupanda mbegu, thamani ya muda pamoja na mavuno ambayo ni matokeo ya
kupanda mbegu.
“Unaweza kuhangaika sana kwa lengo la kupata fedha mbegu, kwa kuwa mbegu hizo zitazalisha
fedha nyingi zaidi kupitia mbegu hiyo”
Semina hiyo iliyowahusisha wanafunzi wa kozi zote chuoni
hapo ikiwemo kozi ya uandishi wa habari,
ualimu,sekretari pamoja na kozi ya kompyuta.
Katika semina hiyo ziliawasilishwa mada kuu tatu na
wakufunzi wa chuo hicho, ambapo mwalimu Onesmo Elia Mbise aliwasilisha mada ya
mikakati ya kibiashara, na mada ya
huduma kwa wateja iliwasilishwa na bw, Christian Ndege na mada ya Miongozo ya
mjasiriamali, iliwasilishwa na Mratibu wa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo
bw, Andrea Ngobole.
Bwana Mayagila alisema kuna kuuuza na kununua lakini sio kila
mtu anaweza kuuza na kuwataka wote kujenga fikra zao katika kuuza ila waweze
kujenga maisha yao
Alisema kama mtu anataka kufanikiwa maishani na kutaka
kununua vitu vya thamani ni lazima mtu ajipange vizuri katika kuuza
“Duniani kuna kuuza na kununua huwezi kukwepa kununua lakini
sio kila mtu anaweza kuuza, unaweza
kuuza mawazo, jambo na bidhaa” Alisema Mayagila
Mayagila aliwashauri wanafunzi wake kujiunga kwenye taasisi za kifedha kwani mkopo ni
fedha mbegu na zitawasaidia kufanikisha
biashara zao na kuzaa zaidi
Amehitimisha ufunguzi wa
semina hiyo kwa kusema kwamba ili mtu yeyote afanikiwe ni lazima kusoma
vitabu mbalimbali
“Nyumba isiyyo na vitabu ni mfu, akili isiyopenda kusoma ni
mfu pia ,ili uweze kufanikiwa nilazima ulipe gharama za kufanikiwa”
Na baada ya uzinduzi huo semina ilianza rasmi ambapo Bw. Onesmo Mbise alifundisha maada ya
Bussiness Planing na kuzungumuzia zaidi mikakati mahususi kuhusu biashara
Bw. Onesmo Elia Mbise akito a maada mapema leo.Picha na Benson Mremi
Mkufunzi wa pili Bw. Christian Ndege yeye alifundisha somo
la Customer Care na kueleza mbinu mbalimbali za kuvutia wateja ikiwa ni pamoja
na kutumia lugha nzuri , kumheshimu na kumtambua kuwa ni bosi na kumwomba radhi
pale tu unapomkosea
Nae kwa upande wake Bw. Andrea Ngobole aliwasilisha somo la
tatu kwa siku ya leo kuhusu misingi/miongozo ya mjasiriamali Bw. Ngobole
amesema mjasiriamali yeyote ni vyema kuwa na marafiki wajasiriamali ili kufanikiwa kupata taarifa
mbalimbali kuhusu Biashara
Bw. Andrea Ngobole Akiwasilisha maada juu ya muongozo wa misingi ya mjasiriamali . Picha na Benson Mremi
Wakati huo huo pia ametaja mambo ambayo mjasiriamali anapaswa kuyaepuka ikiwa ni pamoja na kulaumu, starehe, kuamini uchawi, umbea na mengine mengi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kufika mbali na kufanikiwa kibiasharaBaadhi ya Wanafunzi wa chuo cha AJTC wakiwa makini kufufuatlia moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina ya Ujasiriamali mapema jana
Aidha wanafunzi walio wengi chuoni hapo wameipoke kwa furaha semina hiyo ambayo
itaendelea tena mapema kesho asubuhi saa 3 kamili
credit: this is habari blog
Post a Comment