Ni katika hali ya kuikumbusha jamii umuhimu wa mazazi katika
maisha ya kila siku hasa kwa upande wa mama ambapo Mkundi Production imeandaa tamasha
kubwa la injili ambalo linajulikana kama upendo kwa mama.
Tamasha hilo ambalo litafanyika mwezi wa 11 katika viwanja
vya Shekh Abed Jijini Arusha litahuduriwa na waimbaji mbalimbali maarufu wa
nyimbo za injili kama vile Upendo Nkone,Christina Shusho,Martha Mwaipaja,Baraka
Massa,Eng Carlos, Sarah K kutoka Kenya Pamoja na mama wa Chaguo langu.
Lengo hasa la Tamasha hilo ni kuwasaidia Wakina mama ambao
wanaishi katika mazingira magumu, Ikiwemo kuwapatia mtaji ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na
kumudu gharama za maisha.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mkundi Production yenye
maskani yake Mkoani Arusha Njiro,Engineer Carlos Dionis Mkundi ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili amesema kuwa
amepata msukumo wa kuandaa tamasha hilo ili kuwakumbusha watu kuwa Mama ni
mtu wa kuthaminiwa katika jamii hivyo anapaswa kusaidiwa.
Licha ya hayo pia amesema kuwa jamii nyingi zimekuwa haziwajali wakina mama
wala kuwapa uzito wa heshima unaostahili hivyo ni wakati sasa wa kila mtu
kuhakikisha wanawasaidia wakina
mama,ikiwemo kuwaepusha na majanga ambayo yatapelekea kunyanyasika.
Sambamba na hayo pia katika Tamsha hilo kubwa kabisa kuwai
kutokea katika mkoa huo ikiwashirikisha wasanii kutoka Kenya na Tanzania Pia
Matumaini na Kiwewe watatumbuiza siku hiyo pamoja na ibaada ya kuwaombea Wakina
Mamama.
Post a Comment