PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ARUSHA KUTIKISWA NA TAMASHA LA UPENDO WA MAMA 2 NOVEMBA 2014
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na Tamasha kubwa la upendo kw...
 



Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na Tamasha kubwa la upendo kwa mama linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid tarehe 02-11-2014

Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha radio five cha jijini Arusha akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90
Engineer Carlos Mkindi mwenyekiti wa Tamasha la upendo ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akijibu baadhi ya maswali toka kwa  wanahabari katika studio za mkundi production zilizopo njiro mkoani Arusha  

Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa za tamasha la upendo wa mama

Kampuni ya Makundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
Lengo la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
Studio ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top