PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RAISI KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA MWENGE- TEGETA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Sehemu ya barabara ya Mwenge-Tegeta itakayofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete. Rais wa Jamhuri ya Muu...




Sehemu ya barabara ya Mwenge-Tegeta itakayofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta utakaofanyika Oktoba 1, 2014.

Ufunguzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.

Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Taarifa hii imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (CGU), Wizara ya Ujenzi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top