Stori: Gladness Mallya
MWANADADA Jennifer
Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa katika maisha yake hawezi kuwasahau
watoto yatima na kuanzia sasa, kila mwaka lazima asherehekee nao katika
kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Mwanadada Jennifer Kyaka ‘Odama’
Odama
ambaye hivi karibuni alifanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kutoa
misaada ya vyakula na vitenge kwa watoto yatima na walezi wao wa kituo
cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar huku akiangusha sherehe ya nguvu
ndani ya ukumbi wa Vijana na kuungana na watoto hao, alisema huu ni
wakati wa watoto kufurahi naye.
“Nimeshasherekea
sana bethdei baa na marafiki zangu, lakini kwa sasa nimebadilika na
ndiyo nimeanza mwaka huu nitakuwa na watoto yatima kila mwaka
nikikumbuka siku yangu ya kuzaliwa kwani kama hivi wamejisikia faraja
sana kuja kula pamoja na mimi, kucheza muziki pia kuwaona waigizaji
mbalimbali imekuwa ni furaha kwao,”alisema OdamaCREDIT .GPL
Post a Comment