PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAREKANI KUWEKEZA DOLA BILLIONI 14 AFRIKA!!!!!!!!!!!!!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kampuni kadhaa za Marekani, zimeahidi kuekeza dola bilioni 14 barani Afrika hasa katika sekta ya kawi na miundo msingi. Taarifa hii ni kwa m...



Kampuni kadhaa za Marekani, zimeahidi kuekeza dola bilioni 14 barani Afrika hasa katika sekta ya kawi na miundo msingi. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Rais wa Marekani Barack Obama.

Tangazo hilo limetolewa katika mkutano wa kwanza wa viongozi wa Afrika nchini Marekani. Mkutano wenyewe umehudhuriwa na zaidi ya marais 40 wa bara hilo.

Mkutano huu unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na mataifa ya Afrika huku China ikiendelea kuongeza uekezaji wake barani Afrika.

Rais Obama pia aliandaa maankuli ya jioni kwa niaba ya marais hao katika ikulu ya White house.

Mikataba hiyo iliyotangazwa Jumanne, ilijumuisha ushirikiano wa dola bilioni 5 kati ya kampuni ya Blackstone na Aliko Dangote, mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika kwa kuinua miradi ya kawi na miundo mbinu kuisni mwa jangwa la Sahara pamoja na uekezaji zaidi katika miradi ya kawi inayofadhiliwa na Rais Obama.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka White House, mradi wa kawi kwa Afrika, Power Africa, ulipokea mchango wa dola bilioni 12 za ziada kama ahadi ili kuboresha upatikanaji wa kawi barani Afrika.

'Ustawi na maendeleo''

Benki ya dunia, ilitangaza kuwa itawekeza dola bilioni 5 katika miradi ya kawi huku kampuni ya General Electric ikisema imejitolea kuekeza dola bilioni 2 kusaidia miradi ya miundo msingi pamoja na kupiga jeki ustawishaji wa miundo mbinu na upatikanaji wa kawi.

Rais Obama pia alisema kuwa Marekani itatoa dola bilioni saba za ziada ili kufadhili mradi wa kufanya biashara Afrika , na kufikisha ufadhili wa miradi ya maeneleo barani Afria hadi dola bilioni 33.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top