MAPACHA WALIOZALIWA WAKIWA WAMEUNGANA MKOANI GEITA WAFARIKI DUNIA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: MAPACHA WALIOZALIWA WAKIWA WAMEUNGANA MKOANI GEITA WAFARIKI DUNIA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Watoto wawili mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana tumbo na kifua, wamefariki muda mchache baada ya kuzaliwa katika kituo cha afy... Watoto wawili mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana tumbo na kifua, wamefariki muda mchache baada ya kuzaliwa katika kituo cha afya Katoro wilaya ya Geita mkoani Geita. Akizungumza, mama wa watoto hao, Neema Luswetura (23), alisema alijifunga Agosti 6, muda mchache baada ya kufikishwa katika kituo hicho cha afya. Muuguzi wa zamu katika kituo hicho, Joyce Michael akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema walimpokea mwanamke huyo saa 7 usiku akilalamika uchungu, na hivyo kupelekwa wodi ya wazazi na asubuhi alijifungua watoto wenye uzito wa kilo 5.1 wakiwa wameshikana na kufariki. Alisema wakati wa zoezi la kumzalisha, alilazimika kuomba msaada toka kwa mganga wa zamu, Dk. Daniel Izengo ili kunusuru uhai wa mama huyo lakini watoto wake hawakuweza kupona. Dk. Izengo alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na juhudi za kunusuru uhai wa watoto hao zilishindikana, akieleza kitalaam tukio hilo linajulikana (coujoined twins). Kutokana na hali hiyo, Dk. Izengo ameishauru jamii hususani wajawazito kuzingatia ushauri wanaopewa na madaktari.
Post a Comment