Mkurugenzi
Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akisalimiana na Mkurugenzi wa Mji wa
Babati Bw. Omari M. Mkombole alipomtembelea ofisini kwake wakati wa
ziara ya Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu
Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
Mkurugenzi
Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akizungumza na Mkurugenzi wa Mji wa
Babati Bw. Omari M. Mkombole ofisini kwake kabla ya kukutana na Vijana
kwa ajili ya Mafunzo yanayohusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana leo Mjini Babati.
Mkurugenzi
Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akitoa mada kwa wanamafunzo (hawapo
pichani) wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati
kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kulia ni Mkurugenzi
wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole na katikati ni Afisa Maendeleo ya
Vijana Bi. Amina Sanga.
Bw.
Petro Benedict kutoka Kikundi cha Ebenezer Group akichangia mada wakati
wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu Mikopo
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati yaliyoandaliwa na
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Afisa
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada wakati wa Mafunzo ya Vijana wa
Halmashauri ya Wilaya ya Babati (hawapo pichani) kuhusu Mikopo kupitia
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
===== =====
Na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM
Vijana
wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati waaswa kuzingatia Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 ili kuweza kuleta maendeleo katika
Halmashauri ya Mji wa Babati na hivyo kuwa chachu ya maendeleo nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga wakati wa
Mafunzo kwa Vijana kuhusu upatikanaji wa Mikopo kupitia Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana yaliyofanyika leo Mjini Babati.
Akitoa
mada kuhusu Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana Bibi Mtenga amewataka
vijana kujitambua na kujua kuwa wao ni rasilimali muhimu na mchango
mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na Kijamii hivyo kuithamini Sera ya
Vijana inayomtambua kijana kuwa ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15 hadi
35 na kutumia fursa hiyo kupata haki zao kama vijana.
Aidha
Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga amewataka Vijana wa Babati
kuweka jitihada katika uandikaji wa miradi yao kwa kuzingatia muongozo
wa utoaji fedha za mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na
kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi endelevu ambayo itakuwa na sifa
za kupata mikopo hiyo kupitia SACCOS ya vijana ya Halmashauri hiyo.
Kwa
upande Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole amewataka
Vijana wa Babati kutumia fursa hiyo ya kipekee ya kutembelewa na maofisa
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kupewa mafunzo
ya kuwajengea uwezo mzuri wa kuendesha shughuli zao za uzalishaji mali
kwa ufanisi kwani huu ni muda muafaka kwa Vijana kuendeleza vikundi vyao
na kuweza kuimarisha SACCOS ya vijana kwa maendeleo yao na Mji wa
Babati.
Post a Comment