Mtoto mmoja wa miaka
nane, mkazi wa Mjimwema Songea mkoani Ruvuma amefanyiwa ukatili wa kutisha na
Baba yake wa kambo aitwaye Stan Nyoni kwa kumchoma moto mikono yake yote miwili
kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.Jeshi la polisi mkoani Ruvuma bado
linamsaka mtuhumiwa wa unyama huo,Stan Nyoni ambaye alitoroka baada ya kufanya
unyama huo huku mtoto huyo akiwa amelazawa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Ruvuma Songea.
Tukio hilo la kinyama
limewafanya
baadhi ya madaktari na manesi wa hospitali hiyo kumwaga
machozi kutokana na mtoto Nice kufanyiwa kitendo hicho cha kusikitisha cha
kuchomwa moto mikono yake miwili na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Afisa muuguzi msaidizi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Ruvuma Bw. Aidan Ndunguru anasema mtoto huyo
ameumia katika jicho la kulia,mgongoni huku akiwa na majeraha makubwa katika viganja vya
mikono yake miwili ambayo alimwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto.
Post a Comment