Dr. Raynold Mtungahema
Mamlaka
ya mawasiliano nchini, TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia mitando
kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo watakabiliwa
na mkono wa sheria.
Onyo
hilo limetolewa jana mjini Arusha na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya
mawasiliano nchini TCRA, Dkt, Raynold Mtungahema, alipokuwa akitoa
ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu kuenea kwa picha chafu
zinazowadhalilisha watu mbalimbali kwenye mitandao.
Nilipata
kufafanua yakua mtandao au kifaa chochote cha digitali kinapotumiwa
visivyo kinaweza kupelekea mtumiaji kujikuta akifanya uhalifu mtandao.
Mifano katika hili nilipata kueleza, pale mtumiaji anapotumia mtandao
kutukana, kutishia na kudhalilisha wengine mitandaoni anakua amefanya
kinachoitwa "Cyberbullying" ambacho ufafanuzi wa hili unaweza kusomeka "HAPA"
Kwa
nchi za magharibi wamekuwa na kampeni mbali mbali zinazo hamasisha
kutokomeza aina hii ya uhalifu mtandao ambapo takwimu za ITU za mwaka
2013 zilionyesha takriban nusu ya wenye umri kati ya miaka 13 - 17
wamekua wana athirikazaidi na "Cyberbullying".
Kwa
Tanzania hapakua na tofauti, Mitandao imekua ikitumika kusambaza
taarifa za uongo, chuki na kudhalilisha wengine na hata baadhi kutishia
wengine kupitia mitandao (Simu pamoja na Komputa) kitu ambacho ni hatari
sana kwa usalama wa taifa lolote. Hili lilipelekea TCRA kuja na kampeni
ya "Futa delete kabisa" inayo hamasisha kutosambaza jumbe za chuki,
matusi au uongo ili kulinda amani ya Tanzania.
Aidha,
hapo jana Katika muendelezo wa kuhakiki kunakuwa na matumizi salama ya
mitandao Dr. Mtungahema amesema, matumizi ya mitandao ambayo sio sahihi
ni kosa la jinai na hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja na
akawataka wanaochafuliwa
kupitia mitandao wafungue majalada polisi na mamlaka hiyo itasaidia
kuwafuatilia wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Alisema
mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika kuchafua anaishi
uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili ya matumizi yasiyo
sahihi ambayo hayaruhusiwi.
Mtungahema,
amesema atakaebainika anatumia mtandao kumchafua mtu mwingine huyo
amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe mbele ya vyombo vya sheria kwa
kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa mtuhumiwa atakaepatikana na
hatia.
Aliongeza
kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari wahusika wameshatiwa
mbaroni na ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu mamlaka hiyo itaarifiwe.
Nchi
wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki zimeaanza kikao cha siku nne
jijini Arusha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya mawasiliano.
Mwenyekiti
wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO, Dakta Fracis Wangusi,
amesema sekta ya mawasiliano inakabilwa na changamoto mbalimbali ambazo
zinakwamisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa haraka.
Wangusi
ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya,
amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama kutoka mtandao wa analojia
kwenda digital na matumizi ya visumbusi kwa ajili ya luninga.
Aliongeza
kuwa sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya kuwepo gharama kubwa za
matumizi, usambazaji barua na vifurushi kunakofanywa na mashirika ya
posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao haujapangiliwa, matumizi ya
vikwazo vya kuchelewesha huduma ya haraka ya internet.
Alisisitiza kuwa ili kupatikana kwa mafanikio hayo ni kuondoa vikwazo na kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ICT.
Post a Comment