PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: POLISI ARUSHA WAWAAANGUKIA SSRA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
      ASKARI Polisi mkoani Arusha, wameiomba Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuweka mazingira yatakayowaw...
 
 
 
ASKARI Polisi mkoani Arusha, wameiomba Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuweka mazingira yatakayowawezesha kuhamisha mafao yao kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine.
Akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na SSRA, Inspekta Joseph Labia, alisema uzoefu unaonyesha kuna ugumu wa kuhamisha mafao kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine.
“Kuna mifuko ina mafao mazuri kuliko mwingine na wengi tungependa kuwa na hiyari ya kuhamisha mafao yetu, lakini kuna ugumu wa kuruhusiwa kuhamisha. Tunaomba SSRA muweke mazingira mazuri kwa hili kuwezekana,” alisema Inspekta Labia.
Awali Mkurugenzi SSRA, Ansgnar Mushi, alisema hivi sasa wanafanya utaratibu wa kuoanisha kanuni ya ukokotoaji wa mafao ya wastaafu iwe moja kwa mifuko yote, ili kuwezesha watu kuwa huru kuhamisha mafao yao.
Semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa uelewa wa kutosha kuhusu shughuli za mamlaka hiyo pamoja na uendeshwaji wa sekta ya hifadhi jamii nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top