PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WATAFITI WAELEZEA TABIA ZA MBU AENEZAE UGONJWA HOMA YA DENGUE!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Kufuatia ugonjwa wa homa ya dengue kuibuka mkoani Dar es Salaam na baadaye maeneo mengine ya nchi, wananchi wamek...



 
 








Kufuatia ugonjwa wa homa ya dengue kuibuka mkoani Dar es Salaam na baadaye maeneo mengine ya nchi, wananchi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi yenye utata ambayo sasa yamepata majibu ya wataalamu.
Mtafiti wa tabia za mbu kutoka Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI), Dk Nicholaus Govela amesema mbu anayeambukiza homa ya dengue, Aedes Egypti, hawezi kubeba vimelea vya malaria wala yule anayeambukiza malaria hawezi kuambukiza dengue kutokana na maumbile yao.

Dk Govela amesema fiziolojia ya mwili wa mbu haiwezi kuruhusu Aedes Egypti kubeba virusi vya mbu mwingine.Ndiyo maana mbu hawezi kuambukiza Virusi vya Ukimwi.
Aidha Dk Govela amesema suala hilo bado linahitaji utafiti zaidi kwa sababu kati ya aina tatu za mbu wanaosababisha dengue, hakuna utafiti uliofanyika kujua tabia zao wote.
Amebainisha kuwa katika tafiti zilizofanywa na wataalam mbalimbali kuhusu mbu aina ya Aedes Egypti, Aedes Albokictus na Aedes Africaans., imebainika kuwa Aedes African ndiye anaambukiza dengue na huuma zaidi usiku.
Alisema wengi wanamwelezea mbu huyu kwa kumlinganisha na tabia za mbu wa Japan, China na America ya Kusini lakini inawezekana huyu aliyepo hapa ni mpya tofauti na wa nchi za nje.

Hatahivyo Dk Govela amesema zipo sababu zamsingi kuendelea kufanya  utafiti zaidikwakuwa upo uwezekano wa mbu hawa kujenga usugu wa dawa kwakuwa wamekuwaponchini kwa miaka mingi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top